Na Mwandishi Wetu
MKURUGENZI Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Ephraim Mafuru, ameupongeza uongozi wa Kampuni ya Event and Promotion, kwa kuandaa mbio za Kitulo Garden Marathon, ambazo zimesaidia katika kukuza utalii wa nchi pamoja na kurudisha kwa jamii.
Mafuru amesema ni vyema wadau mbalimbali wakaendelea kujitokeza na kufanya bunifu mbalimbali zenye tija, ili kuleta maendeleo kwa jamii na nchi kwa ujumla.
Akizungumza mapema leo Mei 2,2026 kwenye mbio za Kitulo Garden Marathon, zilizofanyika katika Hifadhi ya Kitulo iliyopo katika Wilaya ya Makete mkoani Njombe, Mafuru aliyemwakilisha mgeni rasmi Waziri wa Maliasili na Utalii, Ashatu Kijaji, amesema utalii wa michezo umeendelea kuwa injini mpya ya kuongeza mapato kwa jamii.
Amesema mbali na utalii wa michezo uliofanyika, vilevile wananchi wengi wamejipatia kipato kwa kuuza bidhaa na kutoa huduma mbalimbali kama huduma ya malazi, vyakula, vinywaji, kazi za mikono na huduma za usafiri hali hii inaonyesha kwamba utalii ni jumuishi.
Aidha, Mafuru ameongeza kuwa marathon hiyo pia imechangia kurudisha kwa jamii kwa kutoa kompyuta 40 zitakazotolewa katika shule nane za sekondari zinazopatikana katika wilaya ya Makete.
"Hali hii inachagiza vitu vinne muhimu ambavyo ni unakimbia, unatangaza, unahifadhi lakini pia unasaidia kwa jamii, hii itaongeza ushiriki wa jamii katika kuhifadhi maliasili", amesema Mafuru.
Kwa upande wake Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi TANAPA Godwell Meing’ataki, ambaye ni Mkuu wa Kanda ya Kusini amesema tukio hilo limefungua fursa kwa wajasiriamali na kuwafanya wananchi kutambua umuhimu wa hifadhi hiyo.
Ameongeza kuwa kiingilio walichotoa washiriki hao zaidi ya 300 kimeongeza mapato kwa Serikali na kukuza uchumi, fedha ambazo zitatumiwa na Serikali katika kuimarisha sekta mbalimbali nchini.
Awali Mratibu wa Marathon hiyo Mony Luvanda, amesema, Marathon hiyo imelenga kujenga utamaduni wa kufanya mazoezi mara kwa mara, kuitangaza hfadhi ya taifa Kitulo pamoja na kufungua fursa ya kuitangaza wilaya ya Makete, huku ikichochea ongezeko la mapato kwa jamii zinazozunguka hifadhi hiyo na wilaya ya Makete kwa ujumla.
Kitulo Garden Marathon imehusisha mbio za kilomita 5, 10 na 21, zikivutia washiriki wengi na kuleta ushindani wenye tija. Ambapo washindi wa mbio hizo walizawadiwa zawadi mbalimbali, huku washindi watatu wa kwanza kupewa fursa ya kulala na kutalii hifadhi ya Taifa ya Kitulo pamoja na wenza wao kwa muda wa siku mbili.

.jpeg)
.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...