NA MWANDISHIWI WETU – MASVINGO – ZIMBABWE

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Kaspar Mmuya (Mb), amewasili nchini Zimbabwe kushiriki Mkutano wa Sita (6) wa Kawaida wa Kamati ya Mawaziri Wanaohusika na Usimamizi wa Maafa kwa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu Mheshimiwa Profesa Palamagamba Kabudi unaofanyika Masvingo, Zimbabwe kuanzia tarehe 11 haadi 14 Mei, 2026.

Mara baada ya kuwasili, Mhe. Mmuya amepokelewa na Balozi wa Tanzania nchini humo, Mhe. Balozi Suzan S. Kaganda na kuipongeza Tanzania kushiriki katika mkutano huo unaolenga kujadili maendeleo yaliyopatikana katika utekelezaji wa programu za kikanda na masuala ya kimkakati katika utekelezaji wa afua mbalimbali katika Usimamizi wa maafa kwa nchi za SADC.

Masuala mengine yaliyoelezwa na Mheshimiwa Balozi Suzani ni  pamoja na Tanzania kuendelea kuzitangaza fursa zilizopo ikiwemo sekta ya utalii, uchukuzi pamoja na kilimo  huku akiahidi kuendelea kuimarisha ushirikiano uliopo baina ya Tanzania na Zimbabwe.

Sambamba na hayo, mkutano huo utahudhuriwa na wadau mbalimbali wa masuala ya Usimamizi wa Maafa kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ambapo ni fursa kwa Tanzania kuendelea kujitangaza Kimataifa kwa kuwa na mifumo thabiti ya Usimamizi wa Maafa pamoja na  kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya Menejimenti ya maafa.

Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizoshiriki katika Mkutano huo wa siku Nne ambapo umekutanisha wadau wa  masuala ya maafa kutoka nchi kumi na sita wakiwemo wataalamu kutoka  katika ngazi za Kimataifa pamoja na Mashirika ya Umoja wa Kimataifa.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...