Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), kwa kushirikiana na Benki Kuu ya Tanzania (BOT), imeandaa semina ya pamoja uliyowakutanisha wataalamu wa Uhasibu, Wakaguzi wa hesabu na wadau wa sekta ya fedha kutoka ndani na nje ya nchi iliyoanza tarehe 25 hadi 27, Mei, 2026.
Akifungua rasmi semina hiyo iliofanyika jijini Arusha, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Emmanuel Tutuba, amewataka wataalamu wa fedha na Ukaguzi nchini kuhamasisha matumizi ya mifumo ya kidijitali katika miamala ya kifedha ili kupunguza matumizi ya fedha taslimu pamoja na vihatarishi vinavyoweza kujitokeza katika sekta ya fedha.
Tutuba amesema matumizi makubwa ya teknolojia katika huduma za kifedha yataisaidia Tanzania kudhibiti uvujaji wa fedha, kuongeza uwazi wa miamala na kuimarisha usalama wa mifumo ya kifedha nchini.
Ametoa wito huo katika semina ya pamoja ya wataalamu wa Uhasibu na Ukaguzi wa hesabu (NBAA) inayofanyika Jijini Arusha, akisisitiza umuhimu wa kusimamia masuala ya mabadiliko ya Tabianchi, mazingira, utawala bora pamoja na vihatarishi vinavyojitokeza kwenye sekta ya fedha kwa kuzingatia viwango vya kimataifa.
Aidha Tutuba amesema Tanzania imeendelea kuwa na uchumi himilivu licha ya changamoto za uchumi wa dunia, huku akibainisha kuwa usimamizi mzuri wa sekta ya fedha na utekelezaji wa mifumo endelevu vitasaidia Taifa kufikia dira ya uchumi wa trilioni moja.
Kwa Upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) CPA Prof. Siasa Issa Mzenzi amesema miongoni mwa mambo watakaojadili na kujifunza ni Pamoja na matumizi ya TEHAMA katika masuala yote ya fedha kupitia.
Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na NBAA na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) yanalenga kuimarisha mfumo wa fedha endelevu kwa kutumia teknolojia sambamba na kuzingatia misingi ya mazingira, kijamii na utawala bora katika sekta ya fedha nchini.
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Emmanuel Tutuba akizungumza wakati wa kufungua semina ya pamoja iliyoandaliwa na NBAA na BOT iliyofanyika jijini Arusha
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) CPA Prof. Siasa Issa Mzenzi akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina ya pamoja iliyoandaliwa na NBAA na BOT iliyowakutanisha wataalamu wa Uhasibu, Wakaguzi wa hesabu na wadau wa sekta ya fedha kutoka ndani na nje ya nchi.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...