Taasisi ya NMB Foundation na Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) zimesaini makubaliano ya utekelezaji wa pamoja wa Mradi wa TIMIZA Malengo, unaolenga kuwawezesha zaidi ya wasichana na wanawake 10,000 katika halmashauri 36 za mikoa 10 kupitia elimu ya fedha, ujasiriamali, stadi za maisha na huduma za kinga dhidi ya maambukizi ya VVU.
Akizungumza jijini Dodoma wakati wa hafla ya utiaji saini, Meneja Mkuu wa NMB Foundation, Nelson Karumuna, alisema afya na uchumi haviwezi kutenganishwa, hivyo mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI yanahitaji kuunganishwa na fursa za kiuchumi kwa vijana, hasa wasichana na wanawake. Alisema NMB Foundation itatumia uwezo na mtandao wa NMB, ikiwemo mawakala zaidi ya 73,000 nchini, kusogeza huduma na maarifa karibu na jamii.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa TACAIDS, Dkt. Adam Mrisho, alisema afya bora kwa vijana ni msingi wa uchumi wa Taifa, hivyo uwezeshaji wa wasichana kwa elimu, stadi za maisha na fursa za kiuchumi ni njia muhimu ya kupunguza mazingira hatarishi yanayoweza kuongeza maambukizi mapya ya VVU.
Dkt. Mrisho alisema Tanzania imepiga hatua katika kupunguza maambukizi mapya kutoka asilimia 0.27 hadi 0.17, lakini akasisitiza kuwa mafanikio hayo yanahitaji ushirikiano endelevu kati ya Serikali, sekta binafsi, taasisi za kiraia na jamii. Makubaliano hayo yanatarajiwa kuimarisha utekelezaji wa Mradi wa TIMIZA Malengo kwa kujenga kizazi chenye afya, ujuzi na uwezo wa kuchangia maendeleo ya Taifa.


.jpeg)

.jpeg)



.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...