Yas Tanzania leo imetambulisha rasmi Yas Business, kitengo maalum kinachounganisha huduma zote za mawasiliano na teknolojia kwa taasisi na biashara chini ya mfumo mmoja wa kisasa.
Hatua hii, ambayo ni uwekezaji wa kimkakati, inaonesha dhamira ya Yas ya kuwaunga mkono wafanyabiashara, wakiwemo wadogo na wa kati (SMEs), pamoja na taasisi za umma na nyingine zote, kutumia teknolojia za kisasa za mawasiliano ili kuongeza ufanisi, kuimarisha utendaji kazi na kuchochea ukuaji wa uchumi wa taifa unaozidi kutegemea mifumo ya kidijitali.
Kupitia Yas Business, taasisi na biashara watanufaika na huduma mbalimbali za mawasiliano ya kisasa na teknolojia zikiwemo mifumo ya kuunganisha matawi ya biashara kwa njia salama na ya haraka ( SD-WAN), huduma za kuhifadhi na kutumia taarifa kupitia mtandao (cloud connectivity), teknolojia ya kuunganisha vifaa na mifumo kupitia mtandao (IoT services), huduma za usimamizi wa mifumo ya mawasiliano (managed solutions) pamoja na kituo cha kisasa cha kuhifadhi na kusimamia taarifa za kidijitali (Tier 3 Data Centre infrastructure).
Huduma hizi ni mahsusi kwa ajili ya kuzisaidia taasisi na biashara kuboresha mawasiliano, kuongeza usalama wa taarifa, kurahisisha utekelezaji wa shughuli za kila siku na kuongeza uwezo wa kukuza biashara kwa ufanisi zaidi.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo Waziri wa Nchi, Mipango na Uwekezaji, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo aliipongeza Yas kwa uwekezaji wake katika miundombinu ya mawasiliano ya kisasa na mifumo ya huduma endelevu za kidijitali, hatua inayochangia kwa kiasi kikubwa azma ya Tanzania ya kujenga uchumi wa viwanda jumuishi.
“Mipango ya uwekezaji kama Yas Business ina mchango mkubwa katika kuongeza uzalishaji, ubunifu na matumizi ya teknolojia katika sekta mbalimbali za uchumi. Ushirikiano kati ya sekta ya umma na sekta binafsi utakuwa msingi muhimu katika kufanikisha Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050,” alisema Waziri Kitila
Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa Yas, Pierre Canton-Bacara, alisema utambulisho wa Yas Business ni mwendelezo wa dhamira ya muda mrefu ya kampuni hiyo ya kuwa mshirika wa kuaminika wa teknolojia kwa taasisi na biashara nchini.
“Yas Business inaunganisha uwezo wetu wa kuhudumia taasisi na wafanyabiashara chini ya mfumo mmoja imara na wa kisasa unaolenga kuongeza ufanisi, kupanua wigo wa shughuli za biashara na kufungua fursa mpya kupitia huduma bora za mawasiliano na teknolojia za kisasa,” alisema Pierre.
Aliongeza kuwa Yas itaendelea kuunga mkono juhudi za Serikali na taifa kwa ujumla katika kukuza uchumi wa kidijitali kwa kuwekeza katika miundombinu na teknolojia zinazochochea ubunifu, kuongeza uzalishaji na kuimarisha juhudi za ujenzi wa taifa.
Yas Business inahudumia sekta mbalimbali muhimu zikiwemo fedha, usafirishaji na ugavi, viwanda, elimu pamoja na huduma za serikali.
Uwekezaji huu unaendana na Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050 pamoja na Mkakati wa Taifa wa Uchumi wa Kidijitali wa mwaka 2024 hadi 2034 (DESF 2024–2034), kwa kuchangia upanuzi wa miundombinu ya mawasiliano ya kisasa, matumizi ya teknolojia katika taasisi na biashara pamoja na ongezeko la uzalishaji.
Ikiungwa mkono na mtandao mpana na imara zaidi nchini Tanzania pamoja na huduma bora kwa wateja, Yas Business ina nafasi nzuri nan kubwa ya kusaidia taasisi na wafanyabiashara kuendesha shughuli zao kwa njia ya kidijitali kwa usalama zaidi, kuimarisha usalama wa mifumo ya taarifa na kuongeza matumizi ya huduma za teknolojia za kisasa.

.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...