Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umeboresha huduma zake kwa kuwarahisishia wanachama kujisajili, kupata taarifa na kufuatilia mafao yao kupitia simu za mkononi bila kulazimika kufika ofisini.

Akizungumza Mei 6, 2026 jijini Dodoma wakati wa mkutano wa wadau wa elimu wa mkoa huo, Meneja wa PSSSF Kanda ya Kati Lulyalya Sayi, amesema maboresho hayo yanalenga kumwezesha mchangiaji kukokotoa mafao yake na kufahamu jumla ya michango aliyowasilisha kwa urahisi zaidi.

Ameeleza kuwa mfuko huo ulianzishwa mwaka 2018 na unahudumia watumishi wa umma pamoja na sekta binafsi, kwa mujibu wa Sayi, PSSSF hutoa mafao ya aina mbili ambayo ni mafao ya muda mfupi na mafao ya muda mrefu.

Amesema Mafao ya muda mfupi yanawalenga wanachama wanaokumbwa na changamoto za muda, ikiwemo wanawake waliojifungua, wafanyakazi waliofukuzwa kazi, pamoja na wagonjwa,ambapo wanufaika hupatiwa mafao kuwasaidia kukabiliana na hali hizo.

Kwa upande wa mafao ya muda mrefu, amesema yanahusisha pensheni ya uzeeni kwa wanachama waliochangia kwa angalau miaka 15, na endapo mchangiaji atafariki baada ya kuanza kupokea pensheni, wategemezi wake watanufaika kwa kipindi cha miaka mitatu kupata mafao yake.

Aidha, mafao ya muda mrefu pia yanajumuisha, Mafao ya warithi, kwa wanachama waliotoa mchango kwa angalau miaka 15 lakini wakafariki kabla ya kustaafu wategemezi wao watapatiwa mafao hayo, lakini pia Mafao ya ulemavu, kwa wanachama wanaopata ulemavu kabla ya kufikia umri wa kustaafu, watapata mafao yao ili mradi wawe wamechangia kwa muda unaostahili.

Kwa sasa, wanachama wanaweza kutumia simu janja kuingia kwenye mfumo wa PSSSF (PSSSF Portal) kupitia google na kupata taarifa za michango  yao kwa urahisi badala ya kufika ofisini, amewataka wananchi kuendelea kujisajili na kufurahia huduma za mfuko huo.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...