Na Pamela Mollel,Arusha
Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt.Juma Homera amesema serikali imechoshwa na tabia ya baadhi ya watu kutumia mitandao ya kijamii kueneza matusi, uchochezi na taarifa zisizo na ukweli dhidi ya serikali na viongozi wake.
Akifungua mafunzo ya siku tatu kwa mawakili wa serikali yaliyofanyika jijini Arusha, Dk Homera amesema tayari orodha ya watu wanaotuhumiwa kujihusisha na vitendo hivyo imewasilishwa Wizara ya Mambo ya Ndani kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria kupitia Jeshi la Polisi.
Kauli hiyo imeungwa mkono na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Damas Ndumbaro ambaye alisisitiza umuhimu wa mawakili wa serikali kushiriki kikamilifu kupambana na upotoshaji unaofanyika mtandaoni.
“Uhuru wa kutoa maoni upo, lakini usitumike kuvunja sheria, kuchochea vurugu au kudhalilisha wengine,” amesema Dk Homera.
Hatua hiyo inaelezwa kuwa sehemu ya juhudi za serikali kuhakikisha matumizi ya mitandao yanafuata maadili, sheria na kulinda amani ya nchi.

.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...