Taasisi ya Saratani Ocean Road imeshiriki katika uzinduzi wa jukwaa la utoaji huduma za afya na bima zinazofanyika katika viwanja vya Posta-TTCL Kijitonyama.
Jukwaa hilo linalenga kuimarisha juhudi za serikali katika kuboresha afya kwa kutoa elimu ya afya kwa jamii.
Pia kuhamasisha kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali pamoja na kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu umuhimu wa kujiunga na huduma za bima ya afya.
Taasisi ya saratani ocean road imepata fursa ya kutoa elimu ya saratani mbalimbali na kuwafanyia uchunguzi wa saratani ya matiti na saratani ya tezi dume kwa wananchi waliofika katika viwanja hivyo.
Aidha taasisi hiyo imewataka wananchi kufika katika viwanja hivyo kupata elimu na kuchunguzwa afya zao bila malipo yoyote.
Jukwaa hilo la utoaji huduma za afya na bima limeanza tarehe 20/05/2026 na linatarajia kumalizika tarehe 24/05/2026.





Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...