Na Said Mwishehe,Michuzi TV
OFISA Maendeleo ya Jamii ambaye ni Mratibu wa Programu ya Kizazi chenye usawa, John Mapunda ameeleza kwamba Tanzania imechagua eneo la haki na usawa wa kiuchumi katika Programu ya Kizazi Chenye Usawa.
Amesema eneo hilo lina mchango mkubwa katika kutatua changamoto mbalimbali za kijinsia nchini huku akifafanua kinara wa utekelezaji ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Mapunda ametoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam wakati wa kikao kazi cha kujadili namna kusuma ajenda ya Kizazi chenye Usawa ,kilichoandaliwa na Shirika la UN Women na kuwashirikisha Wahariri wa vyombo vya habari, waandishi na vijana Generation.
“Katika lengo hilo Tanzania imejiwekea maeneo manne makubwa ya utekelezaji ambayo ni kuongeza huduma za jamii zinazolenga kumpunguzia mwanamke mzigo wa kazi zisizo na malipo, kukuza ajira na kazi zenye staha hususan kwa wanawake, kuongeza uwezo wa wanawake kumiliki rasilimali za uzalishaji ikiwemo ardhi na biashara pamoja na kuandaa bajeti zenye mrengo wa kijinsia.
“Programu ya Kizazi Chenye Usawa ilianza mwaka 2021 na inatarajiwa kukamilika mwaka 2026 .Programu hiyo inatekelezwa Tanzania Bara na Zanzibar chini ya uratibu wa wizara zenye dhamana ya jinsia kwa kushirikiana na UN Women.”
Kwa upande wake Mchambuzi wa Programu za Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi kutoka UN Women, Jackline Chami amesema kwa mwaka huu programu hiyo itajikita katika maeneo saba muhimu.
Ameyataja maeneo hayo ni ustahimilivu wa mabadiliko ya tabianchi, uchumi wa malezi, ujuzi, ujumuishaji wa kidijitali, bajeti na ufadhili wenye mrengo wa kijinsia, kizazi chenye usawa katika taasisi na uendelevu pamoja na ujumuishaji wa watu wenye ulemavu na mabadiliko ya kijinsia.
“Maeneo hayo yanalenga kuongeza ushiriki wa wanawake katika uchumi, teknolojia, maamuzi na kuhakikisha makundi yote yanapata fursa sawa katika maendeleo ya taifa,”amesema alipokuwa akitoa ufafanuzi kuhusu programu hiyo.
Awali Mtaalamu wa Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi kutoka UN Women, Lillian Mwamdanga amesema jukwaa hilo limewakutanisha serikali, mashirika ya kiraia, vijana, sekta binafsi, vyombo vya habari pamoja na washirika wa maendeleo kwa lengo la kugeuza ahadi za usawa wa kijinsia kuwa matokeo halisi kwa wanawake na wasichana.
“Kupitia Jukwaa la Kizazi Chenye Usawa linaloongozwa kwa pamoja na UN Women na wadau mbalimbali duniani, nchi zimekuwa zikitoa ahadi za kifedha na utekelezaji wa programu zinazolenga kuimarisha haki na uwezeshaji wa wanawake na wasichana.
“Tanzania imeonesha uongozi mkubwa kwa kuwekeza katika haki na usawa wa kiuchumi kwa wanawake ambapo tangu mwaka 2021 serikali imekuwa ikitekeleza programu ya kitaifa chini ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Makundi Maalum,”amesema.
Akizumgumzia baadhi ya mafanikio yaliyofikiwa kuwa ni pamoja na kuanzishwa kwa NMB Gender Bond, uwekezaji katika huduma za malezi ya watoto na matumizi ya nishati safi ya kupikia ambayo imesaidia kupunguza mzigo wa kazi kwa wanawake na kuwapa muda zaidi kushiriki shughuli za uzalishaji mali.
Pia amesema ahadi zaidi ya 200 zimepatikana kutoka serikalini, asasi za kiraia, sekta binafsi na taasisi za elimu huku majukwaa 10,000 ya uwezeshaji wanawake yakianzishwa nchini ili kuongeza upatikanaji wa taarifa, fursa za uongozi na mitandao ya kijamii kwa wanawake.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...