Na Mwandishi Wetu
WAKATI vitendo vya uharibifu wa miundombinu katika miradi mbalimbali ya kimkakati ikiripotiwa kuendelea hapa nchini, Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania, (TPDC) limeimarisha ushirikiano na jamii kwa kutoa elimu kuhusu umuhimu wa kulinda na kuhakikisha usalama wa miundombinu ya bomba la gesi asilia unakuwepo.
Katika Programu ya elimu kwa umma inayolenga kuongeza uelewa wa wananchi wanaoishi karibu na maeneo yanayopitiwa na bomba la gesi asilia iliyofanyika hivi karibuni kwenye vijiji vya Mkwalia Kitumbo na Sunguvuni, wilayani Mkuranga mkoani Pwani, maofisa wa shirika hilo wamesema lengo la elimu hiyo ni kuwafanya wananchi wawe sehemu ya mfumo wa ulinzi wa miundombinu hiyo muhimu kwa maendeleo ya taifa.
Akizungumza wakati wa utoaji wa elimu hiyo, Ofisa Mwandamizi wa Maendeleo ya Jamii wa TPDC, Bw. Oscar Mwakasege alisema mpango huo ni sehemu ya mkakati wa muda mrefu wa shirika wa kushirikisha wananchi katika kulinda rasilimali za taifa pamoja na kuhakikisha jamii inakuwa na uelewa sahihi kuhusu matumizi salama ya maeneo yanayozunguka bomba la gesi.
Alisema TPDC imeona umuhimu wa kuwafikia wananchi moja kwa moja katika vijiji vyao ili kuwajengea uwezo wa kutambua viashiria vinavyoweza kuhatarisha usalama wa bomba la gesi na namna ya kuchukua hatua mapema.
“Lengo letu ni kuhakikisha wananchi wanaelewa umuhimu wa bomba la gesi asilia, namna ya kulilinda na kutoa taarifa mapema wanapoona viashiria vya uharibifu au shughuli zisizo salama karibu na miundombinu hiyo. Tunataka wananchi wawe walinzi wa kwanza wa rasilimali hii muhimu ya taifa,” alisema Bw. Mwakasege.
Aliongeza kuwa baadhi ya shughuli zinazoweza kuhatarisha usalama wa bomba la gesi ni pamoja na uchimbaji holela karibu na njia ya bomba, ujenzi usioruhusiwa, uchomaji moto ovyo pamoja na vitendo vya uharibifu wa alama za tahadhari zilizowekwa na mamlaka husika.
Kwa mujibu wa Bw. Mwakasege, usalama wa miundombinu ya gesi asilia una mchango mkubwa katika kuhakikisha huduma mbalimbali muhimu zinaendelea kutolewa nchini, ikiwemo uzalishaji wa umeme kwa kutumia gesi asilia, shughuli za viwandani na maendeleo ya sekta nyingine za uchumi.
Aidha alisema ushirikiano kati ya TPDC na wananchi umeendelea kuleta mafanikio katika maeneo mengi yanayopitiwa na bomba hilo, kwani wananchi wengi wamekuwa wakitoa taarifa mapema kuhusu shughuli zinazoweza kuhatarisha usalama wa miundombinu hiyo.
Katika mikutano hiyo ya elimu, wananchi walipata nafasi ya kuuliza maswali mbalimbali kuhusu usalama wa bomba la gesi, matumizi ya ardhi karibu na miundombinu hiyo pamoja na hatua zinazopaswa kuchukuliwa endapo kutatokea hali yoyote ya hatari.
Wananchi walioshiriki katika mikutano hiyo wameipongeza TPDC kwa kuwafikia moja kwa moja vijijini na kutoa elimu inayosaidia kulinda rasilimali za taifa huku ikijenga uelewa wa pamoja kuhusu masuala ya usalama.
Baadhi yao walisema hapo awali kulikuwa na uelewa mdogo kuhusu umuhimu wa bomba la gesi asilia na madhara yanayoweza kujitokeza endapo miundombinu hiyo itaharibiwa, lakini elimu inayotolewa sasa imewasaidia kuelewa wajibu wao kama sehemu ya jamii inayozunguka mradi huo.
Mwananchi mmoja kutoka kijiji cha Sunguvuni alisema elimu hiyo imewapa mwanga mpya kuhusu umuhimu wa kushirikiana na mamlaka katika kulinda rasilimali za taifa.
“Sasa tunajua kuwa bomba hili lina umuhimu mkubwa kwa taifa na hata kwa maendeleo ya wananchi wenyewe. Tuko tayari kushirikiana na TPDC kuhakikisha miundombinu hii inalindwa wakati wote,” alisema.
Kwa upande wake, uongozi wa vijiji vya Mkwalia Kitumbo na Sunguvuni umeeleza kuwa utaendelea kushirikiana na TPDC katika kutoa elimu kwa wananchi na kuhamasisha jamii kuwa sehemu ya ulinzi wa bomba la gesi.
Utoaji wa elimu kwa umma uaendelea kutekelezwa katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Pwani ikiwa ni sehemu ya juhudi za TPDC za kuimarisha usalama wa miundombinu ya gesi asilia na kujenga mahusiano mazuri kati ya shirika hilo na jamii inayozunguka mradi wa gesi asilia.
TPDC imesisitiza kuwa ushirikiano wa wananchi ni nguzo muhimu katika kuhakikisha miundombinu ya gesi asilia inalindwa kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho pamoja na kuendelea kuchochea maendeleo ya uchumi wa taifa.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...