-Pia yabainisha mkakati wa mageuzi katika mifumo ya utawala na utumishi wa umma
-Utekelezaji Dira 2050 kuanza kutekelezwa rasmi kuanzia Julai 1, 2026
Na Said Mwishehe,Michuzi TV
TUME ya Mipango ya Taifa imeidhinisha miongozo minne itakayotumika katika kusimamia utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 utakaoanza Julai 1 mwaka 2026.
Akizungumza leo Mei 31 katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam,Waziri wa Mipango na Uewekezaji Profesa Kitila Mkumbo amesema miongozo hiyo imetolewa baada ya Tume ya Taifa ya Mipango chini ya Mwenyekiti wake Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kufanya kikao Mei 26 mwaka huu.
“Katika kikao hicho, pamoja na mambo mengine, Tume ya Taifa ya Mipango ilijadili na kuidhinisha miongozo/mikakati minne itakayotumika katika kusimamia tekelezaji wa Dira 2050 utakaonza Julai 1, 2026.”
Profesa Mkumbo ameitaja miongozo hiyo ni Mwongozo wa Kitaifa wa Mipango,Mwongozo wa Kitaifa wa Uidhinishaji wa Miradi ya Maendeleo, Mwongozo wa Kitaifa wa Ufuatiliaji na Tathmini ya Miradi ya Maendeleo,Mkakati wa Mawasiliano wa Dira 2050 wa Miaka Mitano 2026/27 - 2030/31.
“Ilipojadili Muongozo wa Kitaifa wa Ufuatiliaji na Tathmini ya Miradi ya Maendeleo, Tume ya Taifa ya Mipango iliidhinisha maeneo makubwa matatu ya kimkakati yanayohitaji mageuzi yenye viashiria vya upimaji 142.
“Maeneo haya na idadi ya viashiria vyake ya upimaji ni Mageuzi katika mifumo ya utawala na utumishi wa umma (Governance and civil service reforms, viashiria 13), Mageuzi katika uwekezaji na uzalishaji (structural transformation for investment, infusion and productivity, viashiria 53) pamoja na Mageuzi katika maendeleo ya kijamii, kiuchumi na mazingira (socio economic outcomes, viashiria 76)
Ameongeza pia Tume ya TaĆfa ya Mipango ilidhinisha sekta za kipaumbele 12 kama zilivyainishiwa katika Mpango wa Nne wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano yenye viashiria vya upimaji 206
Amefafanua katika sekta ya kilimo idadi ya viashiria vya upimaji katika mabano ni 15, viwanda na ujenzi (10), Madini na Nishati(10), Utalii(5), michezo na Sanaa(9), sekta ya ubunifu na maudhui ya kidigitali(2) wakati sekta ya miliki ,aridhi na maendeleo ya miji(13)
Pia katika sekta ya biashara na uwekezaji(12), Elimu(54), hifadhi za jamii,kazi na ustawi wa jamii(34), uchumi wa bluu(18) pamoja na sekta ya Sayansi,teknolojia,ubunifu na uchumi wa digitali(24).
Akieleza zaidi Profesa Mkumbo ameeleza pia Tume ya Taifa ya Mipango ilielekeza kuwa Sekretariati ya Tume ijielekeze na kujikita katika kusimamia utekelezaji wa mipango ya maendeleo.
Aidha, katika kumarisha simamizi wa utekelezaji wa mipango ya maendeleo, Mwenyekiti wa Tume alielekeza kuwa, wakati ambapo Tume haikutani katika vikao vya kawaida chini yake, wajumbe wa Tume watajigeuza kuwa Ofisi ya Usimamizi wa Utekelezaji wa Mipango (Delivery Bureau) na vikao vyake vitasimamiwa na Makamu Mwenyekiti wa Tume.
Ameongeza Tume ya Taifa ya Mipango ilielekeza kukamilishwa kwa haraka kwa majadiliano kati ya Serikali na wawekezaji kuhusu miradi ya kimkakati ya uwekezaji inayotarajiwa kujenga msingi ya kukuza uchumi na kuchochea ajira kama sehemu muhimu ya utekelezaji wa Dira 2050 na Mpango wa Nne wa Taifa wa Maendeleo ya Miaka Mitano (2026/27 - 2030/31).
Amitaja miradi hiyo ni Mradi unganishi wa chuma cha Liganga na makaa ya mawe ya Mchuchuma, Mradi wa magadi soda wa Engaruka, Mradi wa kuchakata gesi asilia kuwa kimiminika (LNG), Mradi wa nikeli wa Kabanga (Kabanga Nickel Project) na kiwanda cha usafishaji cha Kahama.



.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...