Na Mwandishi wetu, Simanjiro
JUMUIYA ya Wazazi wa CCM Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, imesajili wanachama wapya 16,648 kwa njia ya kielekroniki.

Katibu wa jumuiya ya wazazi wa CCM wilaya ya Simanjiro, Sasi Mirumbe ameeleza hayo kwenye kilele cha maadhimisho ya wiki ya wazazi iliyofanyika kata ya Ruvu Remit.

Mirumbe amesema kuwa kati ya wanachama hao wapya 16,648 wanaume ni 7,319 na wanawake ni 9,165.

Ameeleza kwamba katika uhai wa jumuiya hiyo wamekuwa wakifanya vikao na ziara kwa mujibu wa kanuni na kusajili wanachama wapya.

Amesema kutokana na jumuiya ya wazazi kuhusika na mazingira, malezi ya vijana katika elimu afya na uchumi wa kujitegemea, jukumu ambalo wamekuwa wakilifanya mara kwa mara na vizuri sana.

"Tumekwenda mbali kama jumuiya ya wazazi Simanjiro kwa kutambua baadhi ya watu wazima wasiojua kusoma na kuandika tumekuja na mpango wa darasa mabomani," amesema Mirumbe.

Amesema darasa mabomani ni mpango wa kuwafundisha watu wazima kwenye vitongoji vyao majumbani ili wajue kusoma, kuhesabu na kuandika, kwa kutoa mchango wao wa elimu ya awali, msingi na sekondari kama wazazi.

Amesema ujenzi wa nyumba ya mtumishi, wamefanikiwa kuanza ujenzi ambayo hivi sasa ipo usawa wa madirisha.

"Mhe mgeni rasmi kukamilika kwa nyumba hii kutaendelea kuimarisha jumuiya yetu na chama chetu katika kuongeza rasilimali za kudumu na kupunguza adha kwa mtumishi kupanga pindi yakitokea mabadiliko ya kiutumishi, amesema.

Aidha, amesema nyumba hiyo imesimama kwa muda wa mwaka mmoja kwa kukosa matofali 1,000 ya thamani ya shilingi milioni 1.4 saruji mifuko 50 ya shilingi 900,000 nondo za mm12 shilingi milioni 1 nondo za mm6 za shilingi milioni 1.4 misumari ya shilingi 17,000 mbao shilingi 540,000 binding wire sh 70,000 fedha za fundi shilingi 1.6 jumla shilingi 5,747,500.

Mgeni rasmi wa maadhimisho hayo James Ole Millya ameipongeza jumuiya hiyo kwa namna wanavyotekeleza wajibu wao ikiwemo kuyasema mema yanayofanywa na Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Ole Millya amechangia shilingi 500,000 za ujenzi wa nyumba ya mtumishi na kumuagiza mfanyabiashara maarufu Lesiangiki Mulla kushirikiana na wadau wa maendeleo kukamilisha jengo hilo.

Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi wa CCM Wilaya ya Simanjiro, Haiyo Yamat Mamasita amesema wamekuwa na utaratibu wa kufanya maadhimisho ya wiki ya wazazi katika kata mbalimbali.

Haiyo amesema kwa mwaka 2026 waliamua kupitia vikao kuwa kilele cha maadhimisho hayo yafanyike kata ya Ruvu Remit na mwaka 2027 yatafanyika katika kata nyingine.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...