Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Judith Kapinga, amewashauri Wamiliki wa Viwanda vipya Kutoa kipaumbele kwa wazawa katika ajira ili kukuza uchumi na mapato ya Taifa kwa ujumla.

Akizungumza wakati wa akifungua wa Kiwanda kipya cha kutengeneza tambi za papo hapo (Instant) cha Kura Food mkoani Pwani, amesema kuwa Serikali inaendelea kuboresha mazingira ya Biashara ikiwemo sera, miundombinu, na mifumo ili kuvutia Wawekezaji na wafanyabiashara na kuongeza ushindani wa bidhaa za Tanzania kimataifa.

Aidha, Wizara imefanya mapitio ya sheria na kanuni ili kuhakikisha zinajielekeza katika kuwezesha biashara na kuondoa vikwazo badala ya kudhibiti pekee. Lengo ni kushirikiana na wadau wa mnyororo wa thamani, kutumia teknolojia za kisasa zinazoongeza tija, uzalishaji, na ufanisi wa biashara nchini.

Naye, Mwenyekiti wa Kura Food, Bw. Wu Yeping, ameipongeza Serikali kwa kuweka mazingira rafiki yanayorahisisha uwekezaji,

Huku Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe. Abubakar Kunenge, akibainisha kuanza kwa uboreshaji wa miundombinu ya barabara na Reli ya Kisasa (SGR) kuanzia mwaka ujao ili kufungua zaidi fursa za kibiashara mkoani humo.

Naye Mbunge wa Kisarawe, Mhe. Selemani Jafo, amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa sera zake thabiti ambazo zimekuwa chachu ya kuvutia wawekezaji. Sera hizi zimesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza changamoto ya ukosefu wa ajira kwa wananchi wa jimbo hilo kupitia kuanzishwa kwa viwanda vipya.

            

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...