Na Farida Mangube Morogoro.
Katika juhudi za kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi na uharibifu wa mazingira unaoendelea kuathiri jamii na rasilimali za asili, wadau wa sekta ya mazingira wamekutana mkoani Morogoro kujadili utekelezaji wa Mradi wa RESOLVE NbS (Suluhisho), unaolenga kutumia masuluhisho ya asili kurejesha mazingira yaliyoharibika na kuimarisha maisha ya wananchi.
Semina hiyo imewakutanisha wadau kutoka maeneo mbalimbali yanakotekelezwa mradi huo kwa lengo la kujenga uelewa wa pamoja kuhusu malengo, utekelezaji na matokeo yanayotarajiwa katika kipindi cha miaka mitatu ya mradi huo kuanzia mwaka 2025 hadi 2027.
Mradi wa RESOLVE NbS unatekelezwa kwa ushirikiano wa taasisi mbalimbali zikiwemo Shirikisho la Uhifadhi wa Mazingira Asilia Duniani (IUCN), WWF, CARE, EAMCEF, CAN na CEoT katika mikoa ya Morogoro na Iringa.
Akizungumza katika semina hiyo, Afisa Programu wa IUCN, Abdulaziz Mkwizu, alisema mradi huo umeanza kutekelezwa katika halmashauri tano ambazo ni Ifakara Mji, Mlimba, Morogoro Vijijini, Iringa Vijijini pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo.
Alisema mradi huo utajikita katika kuboresha mipango ya matumizi bora ya ardhi, kurejesha ikolojia za misitu, ardhi na mito iliyoharibiwa pamoja na kuimarisha uwezo wa jamii kupitia vikundi vya kuweka na kukopa (VSLA).
“Mradi huu pia utasaidia jamii kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi kwa kuhamasisha kilimo mseto kinachozingatia bayonuai na kuboresha mifumo ya uzalishaji wa mazao kupitia vyama vya ushirika vya AMCOS,” alisema Mkwizu.
Kwa upande wake, Mratibu wa Mradi kutoka WWF, Josia Japhet Ngamagila, alisema lengo kuu la RESOLVE NbS ni kuhakikisha jamii pamoja na rasilimali za asili zinakuwa na uwezo mkubwa wa kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi kwa kutumia suluhisho zinazotokana na mazingira asilia.
Alisema mafanikio ya mradi huo yatategemea ushirikiano wa karibu kati ya wadau wote wanaoshiriki utekelezaji wake pamoja na ushirikishwaji wa jamii katika maeneo husika.
Ngamagila aliongeza kuwa semina hiyo imekuwa hatua muhimu ya kuwakutanisha wadau mbalimbali ili kuwa na maono ya pamoja katika utekelezaji wa mradi huo unaotarajiwa kuwa chachu ya uhifadhi wa mazingira na maendeleo endelevu kwa jamii za Morogoro na Iringa.
Baadhi ya washiriki wa semina hiyo walieleza kufurahishwa na elimu waliyoipata kuhusu utekelezaji wa Mradi wa RESOLVE NbS, wakisema utasaidia kuongeza uelewa wa jamii juu ya umuhimu wa uhifadhi wa mazingira na matumizi endelevu ya rasilimali za asili.
Walisema kupitia mafunzo hayo wamepata mwanga kuhusu namna bora ya kushiriki katika shughuli za uhifadhi, kilimo kinachozingatia mazingira pamoja na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi katika maeneo yao.
Aidha walitaka kuwepo kwa ushirikishwaji mkubwa wa wananchi katika hatua zote za utekelezaji wa mradi huo ili kuhakikisha manufaa yake yanaifikia jamii moja kwa moja pamoja na kuleta matokeo chanya katika uhifadhi wa mazingira na maendeleo ya kijamii.

.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...