Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa, akiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa Shirika lisilo la Serikali la INADES pamoja na Mratibu wa Kitaifa wa Maadhimisho ya Siku ya Mnyama Punda kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Shabani Tozzo, muda mfupi baada ya ujumbe huo kufika ofisini kwake Mei 20, 2026 jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Serikali la “INADES” Bi. Jacqueline Nicodemus akimkabidhi Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa tuzo ya pongezi leo Mei 20,2026 kwenye ofisi ndogo za Wizara hiyo zilizopo jengo la Kambarage jijini Dodoma kufuatia ushiriki wa Wizara yake kwenye Maadhimisho ya kitaifa ya Punda yaliyofanyika Mei 08,2026 mkoani Geita.
Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Serikali la “INADES” Bi. Jacqueline Nicodemus akimuonesha Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa miongozo mbalimbali ya ustawi wa mnyama Punda muda mfupi baada ya kufika ofisini kwake Mei 20,2026 jijini Dodoma.
Mratibu wa kitaifa wa Maadhimisho ya siku Punda Duniani kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Shabani Tozzo (kushoto) akimkabidhi Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa tuzo ya pongezi iliyotolewa na Shirika lisilo la Serikali la INADES kwa kanda ya Afrika leo Mei 20,2026 kwenye ofisi ndogo za Wizara hiyo zilizopo jengo la Kambarage jijini Dodoma kufuatia ushirikiano uliotolewa na Wizara yake kwenye Maadhimisho hayo yaliyofanyika kitaifa Mei 08,2026 mkoani Geita.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa akiwa kwenye picha ya pamoja na wawakilishi wa Shirika lisilo la Serikali la “INADES” na Mratibu wa kitaifa wa Maadhimisho ya Siku ya mnyama Punda kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Shabani Tozzo muda mfupi baada ya ujumbe huo kufika ofisini kwake Mei 20,2026 jijini Dodoma.






Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...