Wakazi wa jiji la Arusha wanatarajiwa kunufaika na huduma bora zaidi za mawasiliano na intaneti yenye kasi kufuatia uwekezaji mpya wa kampuni ya mawasiliano ya Yas kuongeza minara miwili ya teknolojia ya 5G jijini humo.
Uwekezaji huo umeongeza idadi ya minara ya 5G ya Yas jijini Arusha kufikia 15, huku ikiwa na jumla ya minara (20) ya 4G. Uzinduzi huo ni muendelezo wa kuimarisha upatikanaji wa huduma za mawasiliano ya kisasa zinazolenga kurahisisha shughuli za wananchi na kuchochea maendeleo ya kidigitali katika sekta mbalimbali.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, kwa niaba ya Mkurugenzi wa Yas Kanda ya Kaskazini, Robert Sanyagi - Mkuu wa Yas - Kanda ya Kaskazini alisema kampuni imeendelea kufanya uwekezaji mkubwa wa miundombinu ya mawasiliano ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma zenye kasi, uhakika na viwango vinavyokidhi mahitaji ya dunia ya sasa inayotegemea teknolojia.
“Tunafahamu kuwa huduma bora za mawasiliano zina mchango mkubwa katika kukuza biashara, elimu, afya na huduma za kifedha. Kupitia minara hii mipya, wakazi wa Arusha watanufaika na matumizi bora zaidi ya intaneti yatakayorahisisha shughuli zao za kila siku,” alisema Bw. Sanyagi.
Alisema teknolojia ya 5G itaongeza ufanisi kwa wafanyabiashara wanaotegemea miamala ya kidigitali, vijana wanaojifunza mtandaoni pamoja na wananchi wanaotumia huduma mbalimbali kupitia intaneti.
Kwa upande wake, mkazi wa Arusha, George Shirima alisema uwekezaji huo ni hatua muhimu kwa maendeleo ya jiji hilo kutokana na ongezeko la matumizi ya huduma kidigitali katika shughuli za kila siku.
“Kwa sasa karibu kila kitu kinategemea intaneti, hivyo huduma bora ya mtandao itasaidia sana biashara kukua na vijana kupata fursa zaidi kupitia teknolojia. Huu ni uwekezaji wenye manufaa makubwa kwa wananchi wa Arusha,” alisema, Shirima.
Yas inaendelea kujivunia kuwa miongoni mwa kampuni zinazoongoza kwa uwekezaji wa teknolojia nchini ikiwa na zaidi ya minara 4,800 Tanzania nzima. Kampuni hiyo imesema itaendelea kupanua huduma zake za 4G na 5G ili kuhakikisha Watanzania wengi zaidi wanapata mawasiliano ya uhakika na yenye viwango vya kimataifa.
Robert Sanyagi - Mkuu wa Yas - Kanda ya Kaskazini akizungumza na vyombo vy habari wakati wa hafla hiyo


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...