NA Nasra Ismail, Geita

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martin Shigela, amewataka wananchi kuacha tabia ya kupiga simu za majaribio au mzaha kwenye namba za dharura za Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.

Akizungumza katika kilele cha Siku ya Zimamoto Duniani kilichofanyika kimkoa katika Kata ya Ludete, Katoro, Shigela amesema vitendo hivyo vinaleta usumbufu mkubwa na vinafanya jeshi kushindwa kuamini taarifa za dharura za kweli.

Kufuatia hali hiyo, amewaagiza viongozi wa kata na watendaji kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kuheshimu majukumu ya vyombo vya ulinzi na usalama, hususani Zimamoto, ambacho kinatoa huduma ya moja kwa moja ya kuokoa maisha na mali zao.

Hadi kufikia Mei jumla ya matukio 82 yamepatikana mkoani Geita ambapo matukio ya moto yalikuwa 32, matukio ya maokozi 50 huku jumla matukio yaliyosababisha majeruhi ni 39 na vifo 32.

Kaimu kamanda wa zimamoto mkoa wa Geita Kennedy Mwakasitu ametoa wito kwa jamii kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi Hilo ili liweze kufanya kazi zake kwa ufasaha.

Maadhimisho ya siku ya wazimoto duniani hufanyika Mei 4 ya Kila mwaka ambapo katika mkoa wa Geita yalifanyika katika Mamlaka ya mji mdogo wa Katoro yakiongozwa na matembezi pamoja na elimu juu ya matumizi ya nishati ya kupikia.

Wananchi waliopata Elimu hiyo wameishukuru jeshi la zimamoto kwa namna walivyojufunza namna ya kudhibiti gesi iliyovuja na kuripuka kwa urahisi ambapo hapo awali walikuwa wanapata mshtuko mkubwa unaopelekea maafa makubwa.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...