Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb), amefanya mabadiliko ya kimkakati katika katika Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kwa kumteua Mhandisi Ndele Mengo kuongeza nguvu na kusimamia Idara ya uzalishaji na usambazaji maji DAWASA.

Mhandisi Mengo amepewa dhamana ya kusimamia uzalishaji na usambazaji maji kwa kuhakikisha huduma inaimarika na kukabiliana na changamoto za migao na upungufu wa maji Mkoan Dar ea Salaam na Pwani

Uteuzi huo ni ishara ya dhamira ya dhati ya Waziri Aweso ya kuhakikisha DAWASA inaongeza ufanisi kiutendaji na kufikia malengo ya Serikali ya kutoa huduma kikamilifu kwa Wananchi takribani Milion 7.2 wanaohudumiwa na Mamlaka hiyo.

Katika hatua nyingine, Waziri Aweso amemteua Mhandisi Christopher Gava kuwa Mkurugenzi wa Uwekezaji na Miradi DAWASA.

Akizungumzia mabadiliko hayo, Waziri Aweso amemtaka Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Mkama Bwire, kuendelea kusimamia utendaji kazi na kuchukua hatua kwa watendaji wababaifu watakaoshindwa kutatua changamoto za Wananchi na wasiokuwa na majibu ya utatuzi wa huduma.

“Nimefanya mabadiliko haya ili kuongeza nguvu DAWASA na kuhakikisha tunaimarisha eneo la uzalishaji na usambazaji Maji kwa ambayo ni kipaumbele cha msingi kwa Mwananchi”, amebainisha Mhe Aweso

Amesisitiza kuwa Mhandisi Mengo na timu yake wana jukumu la kuhakikisha uzalishaji unaendana na mahitaji na ratiba za upatikanaji wa Maji zinazingatiwa ili ilete maana halisi ya kumtua mama ndoo kichwani kwa vitendo.

Mhandisi Christopher Gava kuwa Mkurugenzi wa Uwekezaji na Miradi DAWASA.
 Mhandisi Ndele Mengo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...