Na Karama Kenyunko Michuzi Tv
KIJANA,Metson Frank (23) maarufu ‘Mkumbo’ anayeishi Goba Centre wilayani Ubungo amehikumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kosa la kumlawiti mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi 10.
Hukumu hiyo ya kesi ya jinai namba 28576 ya mwaka 2026 imesomwa Jana ya na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Tumsifu Barnabas wa Mahakama Wilaya ya Ubungo.
Kabla ya kusomwa kwa hukumu hiyo, Hakimu Barnabas aliuliza upande wa mashtaka kama walikuwa na lolote la kusema ndipo Wakili wa Serikali Mkuu, Flora Massawe akisaidiana na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Agatha Lumato na Wakili wa Serikali, Clemence Mango waliomba mahakama itoe adhabu kali kwa mujibu wa sheria ili iwe fundisho kwa watu wengine wanaofanya ukatili kwa watoto
"Baada ya kusikiliza ushahidi wa pande zote na kufanya uchambuzi wa kina wa ushahidi uliowasilishwa, mahakama unamtia hatiani mshtakiwa kwa kosa la kulawiti kinyume na kifungu cha 154(1)(a)(2) cha Sheria ya Kanuni za Adhabu, Sura ya 16, Marejeo ya mwaka 2023". Alisema Hakimu
Akisoma hukumu huyo Hakimu Barnabas alisema ushahidi wa mashahidi nane na vielelezo vitatu vilivyowasilishwa mahakamani hapo na upande wa mashtaka umeweza kuthibitisha pasipo kuacha shaka kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo.
Amesema, katika hati ya mashataka ilidaiwa Septemba 10, 2025 majira ya usiku mshitakiwa ambaye ni baba wa kufikia wa mtoto huyo, alitenda kitendo hicho akiwa amelala naye katika chumba kimoja.
Hakimu alisema katika maelezo ya onyo ya mshtakiwa yaliyowasilishwa mahakamani hapo yalidai mshtakiwa alikiri kufanya kitendo hicho kwa kuwa mke wake ambaye ni mama wa mtoto aliyefanyiwa ukatili alikuwa ni mjamzito na hivyo alipata hamu ya ghafla.
Iliendelea kuelezwa kuwa mbali na kumlawiti mtoto huyo, mshtakiwa pia alimpiga na kumchapa kwa waya wa umeme ili asipige kelele wala kulia wakati akimfanyia kitendo hicho hali ambayo ilimuachia majeraha mbalimbali yaliyomlazimu kulazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) kwa muda mrefu.
Aliendelea kueleza kuwa baada ya matibabu, mtoto alipoteza uwezo wa kuona na kuongea.
Akiendelea kuchambua ushahidi wa mashahidi mbalimbali Hakimu Barnabas alieleza kuwa, katika ushahidi wake mama wa mtoto, alidai siku ya tukio walikuwa nyumbani kwa wazazi wa mwanaume eneo la Goba.
Alidai kuwa kutokana na hali yake ya ujauzito, alikwenda kulala huku mume wake akimuomba alale na mtoto huyo katika chumba kingine.
Asubuhi iliyofuata, alibaini kuwa katika chumba alichokuwa amelala mtoto kulikuwa na kinyesi na mtoto alionekana kama anaharisha.
Ilidaiwa kuwa Frank alimweleza hali hiyo mama yake mzazi ambaye walikuwa wanaishi naye, na baada ya kuona mtoto anaendelea kuharisha walimnunulia dawa za kuzuia kuharisha, lakini hali yake iliendelea kuwa mbaya.
Baada ya siku nne, walimpeleka mtoto katika Hospitali ya Taifa Muhimbili akiwa amezimia na kulazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU).
Ilielezwa kuwa uchunguzi wa awali uliofanywa na madaktari ulibaini kuwa mtoto huyo huenda alikuwa amefanyiwa kitendo cha ukatili, kutokana na hali hiyo, madaktari walitoa taarifa katika Kituo cha Polisi Gogoni.
Ilidaiwa askari walifika hospitalini na kuanza uchunguzi mara moja na baada ya uchunguzi Frank alikamatwa nyumbani kwake Goba kwa tuhuma za kumlawiti mtoto huyo.
Hakimu alisema upande wa jamhuri ulihitimisha ushahidi wake na mshitakiwa alikutwa na kesi ya kujibu na katika utete zake alidai kuwa hata yeye alishangaa kuona mtoto ameamka akiwa anaharisha.
Alidai alitoa taarifa kwa watu wa karibu ambao walimshauri mtoto apelekwe hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kwamba baada ya siku tatu alishangaa kukamatwa na polisi kuhusiana na tukio hilo.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...