Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Dodoma
HOSPITALI ya Benjamin Mkapa iliyopo jijini Dodoma imesema inajivunia mafanikio makubwa ambayo imeendelea kuyapata katika utoaji huduma za afya za kibingwa na Ubungo’s bobezi.
Hayo yamesemwa leo Juni 25,2026 na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, Abdallah Baja wakati wa kikao kazi kati ya hospitali hiyo na Wahariri wa vyombo vya habari ambao ni wanachama wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) linaloongozwa na Mwenyekiti wake Deodatus Balile.
Akieleza zaidi amesema hospitali hiyo mwaka 2025 ilitangazwa kuwa hospitali bora zaidi nchini katika kundi la hospitali za rufaa za kanda kwa ubora wa huduma za afya, ikiibuka kinara mbele ya hospitali nyingine kubwa nchini zikiwemo Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya na KCMC.
Aidha, amesema Waziri wa Afya Mohammed Mchengerwa aliwahi kuzielekeza hospitali zote nchini kujifunza kutoka Hospitali ya Benjamin Mkapa kuhusu namna bora ya kuwahudumia wagonjwa, jambo linalothibitisha kiwango cha juu cha huduma zinazotolewa na hospitali hiyo.
Baja alieleza Hospitali ya Benjamin Mkapa ilikuwa hospitali ya pili nchini kuanza huduma za upandikizaji wa figo, huku ikiwa hospitali ya kwanza Tanzania kufanya upandikizaji wa uume (Penile Transplant). Pia ni hospitali ya kwanza ya serikali kufanya upasuaji wa kisasa wa macho na ya pili nchini kufanya upasuaji wa moyo kwa watoto.
Kwa mujibu wa Baja, hospitali hiyo pia imekuwa ya kwanza nchini kutumia mfumo wa hospitali tembezi (Mobile Hospital), ambapo magari maalumu yenye vifaa vya upasuaji, makazi ya wataalamu na vifaa tiba hupelekwa kutoa huduma katika maeneo mbalimbali ndani na nje ya Tanzania. Alisema huduma hizo tayari zimefika katika nchi za Burundi na Malawi.
Akizungumzia historia ya hospitali hiyo, Baja amesema Hospitali ya Benjamin Mkapa ilianzishwa Oktoba 13, 2015 na ilianza na vitanda 40 lakini kwa sasa ina kufika vitanda 600 na inapokea wastani wa wagonjwa zaidi ya 1,200 kwa siku katika huduma za nje.
Ameongeza hospitali hiyo ina majukumu makuu manne ambayo ni utoaji wa huduma za afya, kinga na uhamasishaji wa afya, mafunzo kwa wanafunzi wa kada mbalimbali za afya, pamoja na kufanya tafiti kwa kushirikiana na taasisi za elimu ya juu.
“Tunapokea wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma na vyuo vingine mbalimbali nchini kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo. Ushirikiano wetu na taasisi za elimu na utafiti unatupa uwezo wa kuunganisha nadharia na vitendo kwa manufaa ya wagonjwa,” amesema Baja.
Ameongeza hospitali hiyo kwa sasa inatoa huduma za kibingwa na ubingwa bobezi, zikiwemo huduma za figo, upasuaji wa ubongo, moyo, mifupa na huduma nyingine za kisasa ambazo zimekuwa zikipatikana kwa kiwango cha kimataifa.
Baja ametumia fursa hiyo kuwakaribisha wananchi na wadau mbalimbali kutembelea Hospitali ya Benjamin Mkapa ili kujionea ubora wa huduma zinazotolewa, akisisitiza kuwa hospitali hiyo imeendelea kuwa nguzo muhimu katika kuboresha huduma za afya nchini.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...