WAZIRI wa Viwanda na Biashara Judith Kapinga, amesema Serikali imeendelea kuweka mazingira bora ya uwekezaji na biashara kwa kuboresha sera, sheria na mifumo ya utoaji huduma kuvutia uwekezaji wenye tija.
Kapinga ameyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa chapa mpya ya magari Jetour, jijini Dar es Salaama, ambapo amefafanua uzinduzi huo unaendana kikamilifu na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, Mpango wa Tatu wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano na Ajenda ya Taifa ya Ujenzi wa Uchumi wa Viwanda na Biashara.
Ameongeza uwekezaji huo unadhihirisha dhamira ya kukuza ushiriki wa sekta binafsi, kuongeza matumizi ya rasilimali za ndani,uhamishaji wa teknolojia na kuzalisha ajira kwa Watanzania.
"Tunatambua Africarriers na Jetour hawaleti magari pekee nchini bali wanaleta fursa mpya za biashara, uwekezaji, ajira, maarifa ya kiteknolojia na mchango mkubwa katika maendeleo ya uchumi wa Tanzania na ukanda wetu wa Afrika Mashariki,”amesema Waziri Kapinga.
Pia amewapongeza viongozi wa Africarriers Group na Jetour Global kwa maono yao makubwa kuichagua Tanzania kuwa sehemu ya safari yao ya ukuaji na mafanikio huku akisisitiza Serikali itaendelea kushirikiana na wawekezaji wote wenye nia ya dhati ya kuchangia maendeleo ya Taifa letu.
Akieleza zaidi amesema ujio wa Jetour nchini Tanzania kunafungua ukurasa mpya wa fursa za kiuchumi na uwekezaji huo utazalisha ajira mpya kwa vijana katika maeneo mbalimbali yakiwemo ya mauzo, huduma za kiufundi, ushauri wa huduma kwa wateja, teknolojia ya habari na mawasiliano pamoja na huduma nyingine.
Waziri Kapinga amesema pia mafanikio ya Africarriers kwa kipindi cha zaidi ya miaka 50 ni ushahidi wa uwezo, uthubutu na ustahimilivu wa wafanyabiashara wa Kitanzania.
“Kupitia ushirikiano huo na Jetour, watapiga hatua nyingine muhimu kuelekea Tanzania yenye viwanda imara, ajira nyingi, biashara shindani na uchumi jumuishi kwa kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.”
Kwa upande wa Mkuu wa Idara ya Sheria wa Kampuni za Africarries, Ngasa Mboje amesema kwa mara ya kwanza wameleta gari zinazoendana na soko na mahitaji ya Watanzania kwasababu ni gharama nafuu.
“Magari ya Jetour yanauzwa kwa njia ya malipo ya papo kwa hapo na njia ya mpili ni kwa mkopo kwasababu kuna baadhi ya Watanzania hawawezi kumudu gharama kwa mara kwanza.Hivyo unaweza kununua kwa mkopo na kulipa kidogo kidogo, huku ukiendelea kulitumia gari lako.”
Mgeni rasmi Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Judidh Salvio Kapinga akizungumza mbele ya Wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye hafla ya uzinduzi rasmi wa Chapa mpya ya Magari ya Jetour nchini Tanzania,iliofanyika Juni 8,2026 Masaki, jijini Dar es Salaam
Balozi wa Shirikisho la Urusi nchini Tanzania Mhe. Andrey Avetisyuan akizungumza mbele ya Wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye hafla ya uzinduzi rasmi wa Chapa mpya ya Magari ya Jetour nchini Tanzania,iliofanyika Juni 8,2026 Masaki, jijini Dar es Salaam,ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Judidh Salvio Kapinga
Makamu wa Rais wa Kampuni ya Magari ya Africarriers Group,Bw. Shahid Nabi, akizungumza mbele ya Wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye hafla ya uzinduzi rasmi wa Chapa mpya ya Magari ya Jetour nchini Tanzania,iliofanyika Juni 8,2026 Masaki, jijini Dar es Salaam,ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Judidh Salvio Kapinga
Baadhi ya Viongozi na wageni waalikwa wakishuhudia uzinduzi wa Chapa mpya ya Magari ya Jetour nchini Tanzania,hafla iliofanyika Juni 8,2026 Masaki, jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Makampuni ya Africarriers, Bw. Fida Rashid, akimkabidhi Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China nchini Tanzania, Mhe. Chen Mingjian mfano wa gari ya Jetour iliozinduliwa nchin Tanzania.
Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China nchini Tanzania, Mhe. Chen Mingjian akiwasha gari ya Jetour iliozinduliwa nchini Tanzania hapo jana,Masaki jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi wa Chapa mpya ya Magari ya Jetour nchini Tanzania,hafla iliofanyika Juni 8,2026 Masaki, jijini Dar es Salaam.


.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...