Na Janeth Raphael MichuziTv
Benki ya CRDB imeendelea kuonesha dhamira yake ya kuwekeza katika ustawi wa wafanyakazi kwa kuendesha programu ya Wellness Day jijini Dodoma, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuhakikisha wafanyakazi wanakuwa na afya bora ya mwili, akili na hisia ili kuongeza ufanisi kazini na kuboresha huduma kwa wateja.
Programu hiyo, ambayo imekuwa ikiadhimishwa kwa miaka sita mfululizo, imewakutanisha mamia ya wafanyakazi wa benki hiyo katika viwanja vya Shule ya Sekondari John Merlin, ambapo walishiriki mazoezi ya viungo, michezo mbalimbali, vipimo vya afya pamoja na semina za lishe, afya ya akili na usimamizi wa mtindo bora wa maisha.
Akizungumza baada ya kuwaongoza wafanyakazi katika mazoezi ya viungo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Edward Mpina, amesema afya ya mfanyakazi ndiyo msingi wa utendaji bora wa taasisi, akisisitiza kuwa wafanyakazi wenye afya njema na utulivu wa akili huchangia kwa kiwango kikubwa utoaji wa huduma bora kwa wateja.
Amesema benki imeendelea kuweka ustawi wa wafanyakazi wake katika ajenda za kipaumbele kwa kuwa mafanikio ya taasisi yanategemea nguvu kazi yenye afya, motisha na uwezo wa kutekeleza majukumu kwa ufanisi.
“Tumekuwa mstari wa mbele kuhakikisha wateja wetu wanapata huduma bora wakati wote. Hata hivyo, hilo haliwezi kufikiwa bila kuwa na wafanyakazi wenye afya njema ya mwili na akili. Wellness Day ni sehemu ya mkakati wetu wa kuwapa nafasi ya kupima afya, kupata ushauri wa kitaalamu kuhusu lishe na mtindo wa maisha pamoja na kutatua changamoto zinazoweza kuathiri utendaji wao,” amesema Mpina.
Amebainisha kuwa kufuatia mafanikio ya programu hiyo katika maeneo mbalimbali, Benki ya CRDB itaendelea kuifikisha katika kanda zote nchini na nje ya Tanzania ambako benki hiyo inatoa huduma, ili kuhakikisha kila mfanyakazi ananufaika na mpango huo wa ustawi.
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Benki ya CRDB, Masoud Matange, amesema mazingira ya kazi ya sasa yanaweza kuwafanya wafanyakazi kutumia muda mwingi ofisini na kusahau kujali afya zao, jambo linaloweza kuongeza hatari ya magonjwa yasiyoambukiza pamoja na msongo wa mawazo.
Amesema kupitia Wellness Day, wafanyakazi wanakumbushwa umuhimu wa kufanya mazoezi mara kwa mara, kupata usingizi wa kutosha, kula lishe bora, kufanya vipimo vya afya kwa wakati na kutafuta ushauri wa kitaalamu kuhusu afya ya akili.
“Mafanikio ya Benki ya CRDB yanatokana na mchango wa kila mfanyakazi. Ndiyo maana tunaendelea kuwekeza katika afya na ustawi wao ili waweze kuendelea kutoa huduma zenye ubora wa hali ya juu kwa wateja wetu,” alisema Matange.
Mbali na mazoezi ya viungo na michezo, washiriki walipata huduma za uchunguzi wa afya pamoja na ushauri kutoka kwa madaktari na wataalamu wa afya kuhusu saikolojia, mahusiano, lishe, kinga dhidi ya magonjwa na namna ya kudhibiti msongo wa mawazo.
Programu hiyo ni mwendelezo wa kampeni ya Wellness Day ya mwaka 2026 ambayo ilizinduliwa jijini Mwanza kabla ya kuendelea katika kanda mbalimbali ikiwemo Burundi, Dar es Salaam, Pwani na sasa Kanda ya Kati yenye makao yake Dodoma.
Kupitia mpango huo, Benki ya CRDB inalenga kuwafikia wafanyakazi wake wote katika kanda nane za shughuli zake ndani na nje ya Tanzania, ikiwa na lengo la kujenga nguvu kazi yenye afya, weledi na uwezo wa kutoa huduma bora zinazokidhi matarajio ya wateja.

.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...