Benki ya Equity Bank Tanzania imeungana na wadau mbalimbali katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Biashara Ndogo, Ndogo na za Kati (SME Day) yaliyofanyika katika Ukumbi wa NSSF Mafao House, Ilala, Dar es Salaam, ambapo ilishiriki kama mshirika na mfadhili wa hafla hiyo iliyoandaliwa na SIDO.

Katika hafla hiyo, Equity Bank Tanzania na SIDO zilisaini Hati ya Makubaliano (MoU) ya kimkakati yenye lengo la kuwawezesha zaidi ya wajasiriamali 8,000 nchini Tanzania kupitia huduma za kifedha, mafunzo ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uunganishaji wa masoko, ili kuimarisha ukuaji wa wa biashara ndogo na kati zinazochangia uchumi na ajira nchini 

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Bi. Theresia Aloyce Mayanie, Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wadogo, wa Kati,  na Binafsi kutoka Equity Bank Tanzania, alisema benki hiyo itaendelea kuwa mshirika mkuu wa maendeleo ya wajasiriamali nchini kupitia suluhisho mbalimbali za kifedha. Bi. Theresia alisema: "Equity Bank tunaamini kuwa wajasiriamali ndio injini ya ukuaji wa uchumi. 

Kupitia ushirikiano wetu na SIDO, tunalenga kuwawezesha maelfu ya wafanyabiashara kupata mitaji, maarifa na fursa zitakazowasaidia kukuza biashara zao na kuboresha maisha yao.

Kwa ujumla, benki hiyo imeahidi kuendelea kushirikiana na taasisi za serikali na sekta binafsi ili kuimarisha mazingira ya biashara na kusaidia ukuaji endelevu wa wajasiriamali nchini Tanzania. @equitybanktz








Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...