●Samwel Emmanuel asema gari hilo litamsaidia kumalizia masomo, kuanzisha kipato na kusaidia familia
Na Mwandishi Wetu.
Mwanza,
Tanzania, 26 Juni 2026 – PigaBet imemkabidhi Samwel Emmanuel,
mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika Chuo Kikuu cha SAUT Mwanza, gari aina
ya Toyota IST aliloshinda kupitia kampeni ya Shinda Ndinga.
Makabidhiano
hayo yamefanyika jijini Mwanza, ambako Samwel anaishi na kusoma. Kabla
ya kukabidhiwa gari hilo, Samwel alisafiri kwa ndege kwa mara ya kwanza
kwenda Dar es Salaam kukamilisha taratibu za nyaraka za umiliki.
Samwel,
mwenye umri wa miaka 24, ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu anayesomea
Procurement, Logistics and Supply Chain Management katika SAUT Mwanza.
Ametokea Wilaya ya Busega mkoani Simiyu.
Kwa
mujibu wa Samwel, taarifa za ushindi wake zilipokelewa kwa mshangao
mkubwa na familia yake pamoja na marafiki zake, kwa kuwa hawakuamini
mara moja kuwa ameshinda gari kupitia kampeni hiyo.
“Nilipopigiwa simu, nyumbani hawakuamini,” alisema Samwel. “Baada ya kuthibitisha taarifa, furaha ilikuwa kubwa sana.”
Samwel
alisema mama yake na bibi yake walikuwa wakimpigia simu mara kwa mara
kufuatilia safari yake na kuhakikisha kila hatua inaenda vizuri.
“Bibi na mama hawakulala. Walikuwa wananipigia simu kila mara kujua kama kweli naenda kuchukua gari,” alisema.
Akizungumzia
ushindi huo, Samwel alisema gari hilo ni mwanzo wa hatua mpya katika
maisha yake, hasa baada ya kumalizia miezi miwili iliyobaki katika
masomo yake.
“Najisikia
furaha kubwa sana. Siwezi kuelezea furaha niliyonayo. Namshukuru
Mungu,” alisema Samwel. “Nitamalizia masomo yangu, kisha gari
nitalitumia kwa biashara. Nataka linisaidie mimi na familia yangu.”
Samwel
alisema mpango wake ni kulitumia gari hilo kwenye biashara ya taxi kwa
kuajiri dereva ili liweze kumuingizia kipato. Pia ana ndoto ya kuwekeza
kwenye kilimo na biashara ya mazao, ikiwemo mahindi na mpunga.
Arthur
Kazola, Meneja Masoko wa PigaBet, alisema kampeni ya Shinda Ndinga ni
sehemu ya juhudi za kampuni kuwashirikisha na kuwazawadia wateja wake.
“Tunampongeza
Samwel Emmanuel kwa ushindi huu. Simulizi yake imeonesha namna kampeni
hii ilivyogusa maisha ya mshindi na familia yake. Kwetu, hii siyo tu
makabidhiano ya gari; ni furaha ya mshindi, familia yake na jamii
inayomzunguka,” alisema Kazola.
PigaBet ilimpongeza Samwel na kuwashukuru wateja wote walioshiriki kampeni ya Shinda Ndinga.

Mwakilishi wa PigaBet, Gideon Magana (kushoto), akimkabidhi gari aina ya Toyota IST mshindi wa kampeni ya Shinda Ndinga, Samwel Emmanuel (kulia), ambaye ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine Tanzania (SAUT), jijini Mwanza. Samwel amesema gari hilo litamsaidia kumalizia masomo yake, kuanzisha shughuli za kujiongezea kipato, pamoja na kuisaidia familia yake.
Samwel Emmanuel akifurahia gari lake aina ya Toyota IST baada ya kukabidhiwa rasmi na PigaBet jijini Mwanza kupitia kampeni ya Shinda Ndinga.
Gideon Magana, mwakilishi wa PigaBet (kushoto) akimkabidhi Samwel Emmanuel, mwanafunzi wa SAUT Mwanza, nyaraka za gari aina ya Toyota IST aliloshinda kupitia kampeni ya Shinda Ndinga ya PigaBet, jijini Mwanza.




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...