Kampuni ya HQ Tanzania imetoa msaada wa vifaa tiba kwa watoto wenye ulemavu wanaolelewa na Kituo cha SBHD Foundation, hatua inayolenga kusaidia ustawi na kuboresha maisha ya watoto wenye mahitaji maalum.
Akizungumza baada ya kupokea msaada huo, Mkurugenzi wa SBHD Foundation, Suma Geofrey, alisema vifaa hivyo vitasaidia kuimarisha huduma zinazotolewa kwa watoto hao na kuchangia katika juhudi za kuwawezesha kuishi kwa kujitegemea zaidi.
Alitoa shukrani kwa uongozi wa HQ Tanzania kwa mchango huo, akisema ushirikiano kati ya sekta binafsi na taasisi zinazohudumia makundi maalum una nafasi muhimu katika kuimarisha ustawi wa jamii.
Suma pia alitoa wito kwa wadau mbalimbali na wananchi kuendelea kushiriki katika kusaidia watoto wenye mahitaji maalum kupitia michango na huduma mbalimbali zinazoweza kuboresha mazingira yao ya maisha na kujifunzia.



.jpeg)
.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...