Na Pamela Mollel,Arusha
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM anayeshughulikia Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Kenani Laban Kihongosi, anaanza ziara maalum ya siku tatu mkoani Arusha kuanzia Juni 4 hadi 6, 2026, kwa lengo la kusikiliza kero za wananchi, kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kuimarisha uhai wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika ngazi zote
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha, Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi wa CCM Mkoa wa Arusha, Saipulani Ramsey, amesema ziara hiyo ni fursa adhimu kwa wananchi kufikisha changamoto zao moja kwa moja kwa viongozi wa chama na Serikali ili zipatiwe ufumbuzi wa haraka.
Ramsey amesema Kihongosi pamoja na ujumbe wake watatembelea na kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, kwa lengo la kujionea maendeleo yaliyofikiwa na kupokea maoni ya wananchi kuhusu ubora wa huduma zinazotolewa
Ameeleza kuwa sekta za elimu, afya, maji na miundombinu ni miongoni mwa maeneo yatakayopata kipaumbele katika ziara hiyo, huku viongozi wakitarajiwa kukusanya maoni na mapendekezo yatakayosaidia kuboresha zaidi utoaji wa huduma kwa wananchi
Mbali na masuala ya maendeleo, ziara hiyo itahusisha tathmini ya uhai wa CCM kuanzia ngazi ya matawi hadi mkoa, pamoja na mikutano na wanachama na viongozi wa chama kwa ajili ya kujadili utekelezaji wa maelekezo mbalimbali ya chama.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa, Kihongosi ataanza ziara yake Wilaya ya Karatu Juni 4, kisha kuelekea Arumeru Juni 5, kabla ya kuhitimisha kwa mkutano mkubwa wa hadhara katika Jiji la Arusha Juni 6
Wakati huo huo, CCM Mkoa wa Arusha imesema imeendelea kuimarisha chama katika maeneo mbalimbali ambapo tayari imefikia kata 107 kati ya kata 161 kupitia ziara inayoongozwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha, Thomas Ole Sabaya. Chama hicho kimesema mwitikio wa wananchi umekuwa mkubwa na umechangia kutatua changamoto mbalimbali za maendeleo katika jamii.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...