Na Mwandishi Wetu

TANZANIA imeshiriki kikao cha Kamati ya Utekelezaji wa Viwango vya Kazi kinachoendelea jijini Geneva, Uswisi, ikiwa ni sehemu ya Mkutano Mkuu wa 114 wa Shirika la Kazi Duniani (ILO).

Katika kikao hicho kilichifanyika leo Juni 2, 2026 ambapo wajumbe wamejadili masuala mbalimbali yanayohusu utekelezaji wa viwango vya kazi, ikiwemo mjadala wa jumla kuhusu ripoti kuu ya Kamati ya Mkutano na maadhimisho ya miaka 100 ya ajenda ya Kazi zenye Staha, Tathmini ya Jumla, pamoja na wajibu wa nchi wanachama katika kuwasilisha taarifa na kutekeleza majukumu mengine yanayohusiana na viwango vya kazi.

Ujumbe wa Tanzania katika kikao hicho ulijumuisha Jaji wa Mahakama ya Rufani Dkt. Yose Joseph Mlyambina, Kamishna wa Kazi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano Kazini, Suzan Mkangwa, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali Pa Kazi (OSHA), Khadija Mwenda, pamoja na Mkurugenzi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA), Usekelege Mpulla

Tanzania, ambayo ni mwanachama wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) na mjumbe wa Bodi ya Magavana inayowakilisha nchi za Ukanda wa Afrika Mashariki, inaendelea kushiriki Mkutano Mkuu wa 114 wa shirika hilo unaowakutanisha wawakilishi wa Serikali, Waajiri na Wafanyakazi kutoka nchi wanachama 187.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...