Benki ya NMB imetangaza udhamini wa Sh milioni 150 kufanikisha msimu wa nane wa Mashindano ya Kombe la Mkuu wa Majeshi—CDF Cup 2026—yatakayofanyika Dar es Salaam kuanzia Julai 6 hadi 17.

Mashindano hayo yatahusisha michezo 13 na timu kutoka Kamandi ya Makao Makuu ya JWTZ, Kamandi ya Jeshi la Nchi Kavu, Kamandi ya Jeshi la Anga, Kamandi ya Jeshi la Wanamaji, Kamandi ya Jeshi la Akiba na Kamandi ya Jeshi la Kujenga Taifa.

Mkuu wa Idara ya Wateja Binafsi wa Benki ya NMB, Aikansia Muro, alisema udhamini huo unaendeleza ushirikiano wa benki hiyo na majeshi katika kukuza michezo, kuimarisha ushindani na kujenga umoja, afya thabiti na mshikamano miongoni mwa washiriki.

Mashindano yatafunguliwa Julai 6 katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, huku yakitarajiwa kutoa jukwaa la kukuza vipaji, kuimarisha utimamu wa mwili na afya ya akili pamoja na kujenga mahusiano mema kwa washiriki.


Mkuu wa Idara ya Wateja Binafsi wa Benki ya NMB, Aikansia Muro (kushoto), akikabidhi hundi mfano ya udhamini wa Sh milioni 150 kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya CDF Cup 2026, Brigedia Jenerali Saidi Hamis Saidi (katikati), jijini Dar es Salaam. Mashindano hayo yatafanyika kuanzia Julai 6 hadi 17, yakishirikisha timu za kijeshi katika michezo 13.

























Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...