Mkurugenzi wa Kadama English Medium Primary School, Leticia Pastory, ameibuka mshindi wa Tuzo ya Mmiliki Bora wa Shule wa Kike Mkoa wa Geita kwa mwaka 2026. Tuzo hiyo imetolewa kwa kutambua mchango wake mkubwa kwenye sekta ya elimu.

Tuzo ilikabidhiwa rasmi Juni 6, 2026 na Mwenyekiti wa UWT Taifa na Mbunge, Mary Chatanda, kwenye Tamasha la Mwanamke wa Dhahabu 2026 lililofanyika Golden Social Hall, Geita. Tukio hilo liliandaliwa na Geita Women and Youth Foundation inayoongozwa na Mkurugenzi Cecylia Miraji.

Hafla hiyo muhimu ilihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa Martine Shigela, Mbunge wa Geita Mjini Chacha Wambura, na Mkurugenzi wa Manispaa Yefred Myenzi.

Baada ya kupokea tuzo, Leticia alisema mafanikio hayo yanatokana na jitihada za miaka mingi za kuinua elimu Geita. Alibainisha kuwa Kadama imejijengea heshima kitaifa kutokana na matokeo mazuri na mazingira bora ya masomo.

Alikumbusha kuwa mwaka 2018 shule hiyo iliweka historia baada ya mwanafunzi wake kushika nafasi ya kwanza kitaifa na mwingine wa pili kwenye matokeo ya darasa la saba.

"Ni faraja kubwa. Tuzo hii inatupa nguvu kuendelea kutoa elimu bora na kuhamasisha wanawake wenzangu watumie nafasi zao kuleta mabadiliko," alisema Leticia.









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...