Zaidi ya wanaushirika 2,000 wamepata mafunzo ya ushirika na maendeleo binafsi kupitia Jukwaa la Tano la Maendeleo ya Ushirika Mkoa wa Dodoma lililofanyika Juni 5 hadi 6, 2026 jijini Dodoma, likiwa na lengo la kuwakutanisha wadau wa ushirika kujadili mafanikio, changamoto na fursa za maendeleo katika sekta hiyo.

Akizungumza wakati wa kuwasilisha taarifa ya maendeleo ya ushirika mbele ya mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. David Silinde, Mrajisi Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Dodoma, Joseph Chintika, Juni 6, 2026.

Amesema ushirika utaendelea kuwa na tija iwapo wanachama watazingatia uadilifu, utoaji wa huduma bila ubaguzi pamoja na kuhakikisha mazao yanayouzwa yanakuwa safi na yenye ubora, ikiwa ni moja ya nyenzo muhimu katika kuwasaidia wakulima kupata bei nzuri na kuongeza ushindani wa bidhaa zao katika soko.

Katika hatua nyingine, Chintika amesema matumizi ya mifumo ya kidijitali katika vyama vya ushirika mkoani Dodoma yameongezeka kutoka vyama 40 hadi 60, sawa na ongezeko la asilimia 23, hatua ambayo imechangiwa na juhudi za kuhamasisha matumizi ya teknolojia katika usimamizi wa shughuli za ushirika.

Aidha, amesema usajili wa wanachama umeongezeka kwa asilimia nne kutokana na mwamko unaoendelea kutolewa kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kujiunga na vyama vya ushirika.

Ametoa shukrani kwa Mrajisi Mkuu wa Vyama vya Ushirika nchini kwa mchango wake katika kuimarisha na kukuza sekta ya ushirika nchini, hali ambayo imewezesha vyama vingi kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma kwa wanachama.

Kwa mujibu wa Chintika, Mkoa wa Dodoma una jumla ya vyama vya ushirika 127 vinavyojumuisha SACCOS, vyama vya mazao na vyama vingine vya ushirika, vyenye jumla ya wanachama 22,228.

Amesema hadi sasa vyama 82 kati ya hivyo vimefikiwa na kupewa elimu mbalimbali za ushirika kwa lengo la kuongeza ufanisi, uwajibikaji na tija katika shughuli zao za kila siku.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...