-Wananchi wa zaidi 400 wapata elimu ya uhifadhi wa mazingira kutoka NEMC Dodoma.
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Zaidi ya wananchi na wadau 400 wametembelea banda la Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) na kupata elimu kuhusu uhifadhi wa mazingira katika maadhimisho ya Wiki ya Mazingira Duniani yaliyofanyika jijini Dodoma.
Meneja wa Kanda ya Kati wa NEMC, Novatus Mushi, amesema mwitikio huo unaonesha kuongezeka kwa uelewa wa wananchi kuhusu umuhimu wa kuhifadhi mazingira na mchango wa elimu katika kubadili mitazamo ya jamii kuelekea maendeleo endelevu.
Akizungumza katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yaliyofanyika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Centre (JKCC) Juni 5, 2026, Mushi alisema NEMC imeendelea kutumia mifumo ya kisasa ya kidijitali katika kusimamia na kufuatilia mazingira kwa wakati halisi.
Alisema miongoni mwa mifumo hiyo ni teknolojia inayowezesha kutambua viashiria vya uchafuzi wa mazingira mara vinapotokea, hatua inayorahisisha ufuatiliaji na kuchukua hatua stahiki kwa wakati.
“Tunazo mifumo ya kisasa ya usimamizi wa mazingira ya kidijitali. Mfumo huu mpya unatuwezesha kuona dalili za uchafuzi wa mazingira kwa wakati halisi na hivyo kuongeza ufanisi katika usimamizi wa mazingira,” alisema Mushi.
Aidha, alisema NEMC inaendelea kutumia Mfumo wa Usimamizi wa Miradi (PMS) unaorahisisha utoaji wa vibali vya Tathmini ya Athari kwa Mazingira (EIA) kwa miradi mbalimbali ya maendeleo kabla ya kuanza kutekelezwa.
Kwa mujibu wa Mushi, matumizi ya mifumo hiyo yamechangia kuongeza uwazi, kupunguza muda wa utoaji huduma na kuimarisha usimamizi wa mazingira nchini.
Amesema maonyesho hayo yamewapa fursa wadau na wananchi kujifunza namna teknolojia inavyoweza kutumika katika kulinda mazingira na kuhimiza maendeleo yanayozingatia uhifadhi wa rasilimali za asili.
Mushi pia alisema NEMC inaendelea kushirikiana na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) katika kubadilishana taarifa na takwimu za hali ya hewa na mazingira ili kusaidia kupanga na kutekeleza miradi kwa kuzingatia athari za mabadiliko ya tabianchi.
Alieleza kuwa ushirikiano huo unasaidia kufanya maamuzi sahihi ya maendeleo na kuzuia hasara kubwa za kiuchumi ambazo zinaweza kujitokeza endapo miradi itatekelezwa bila kuzingatia taarifa muhimu za hali ya hewa na mazingira.
Akizungumzia mwelekeo wa NEMC kuwa mamlaka kamili, alisema hatua hiyo itasaidia kuimarisha ufanisi wa utendaji kazi, kupunguza urasimu na kuongeza kasi ya utekelezaji wa majukumu ya usimamizi wa mazingira.
“Mazingira, watu na uchumi lazima viendane. Tukipata mamlaka kamili tutaongeza ufanisi wa utendaji kazi na kuboresha huduma kwa wananchi,” alisema.
Hata hivyo, alisema Kanda ya Kati inayojumuisha mikoa ya Dodoma, Singida na Iringa bado inakabiliwa na changamoto mbalimbali za mazingira, ikiwemo migogoro ya matumizi ya ardhi, matumizi ya teknolojia duni katika shughuli za kiuchumi na uelewa mdogo wa baadhi ya wananchi kuhusu umuhimu wa uhifadhi wa mazingira.
Alisema NEMC itaendelea kuimarisha utoaji wa elimu kwa umma, usimamizi wa sheria za mazingira na ufuatiliaji wa shughuli mbalimbali ili kuhakikisha rasilimali za mazingira zinahifadhiwa kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.

.jpeg)

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...