Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha imetoa mikopo yenye thamani ya Shilingi milioni 991.5 kwa vikundi 51 vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu katika robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2025/2026, hatua inayolenga kuongeza fursa za kiuchumi, kupanua biashara na kupunguza umaskini kwa wananchi.
Mikopo hiyo imetolewa katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ambapo jumla ya Shilingi milioni 359 zilitolewa kwa vikundi 17 vya wanawake, Shilingi milioni 557 kwa vikundi 25 vya vijana na Shilingi milioni 75 kwa vikundi tisa vya watu wenye ulemavu.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini, Mhe. Silvestry F. Koka, amesema mikopo ni nyenzo muhimu ya kuwawezesha wananchi kujikwamua kiuchumi, hasa kwa kuzingatia kuwa wengi hukosa mitaji kutokana na masharti magumu ya taasisi za kifedha.
Amesema Halmashauri inapaswa kuendelea kutoa mafunzo ya ujasiriamali na usimamizi wa fedha ili kuhakikisha walengwa wanatumia mikopo hiyo kwa tija na kurejesha kwa wakati.
“Wapo wananchi wenye uwezo wa kufanya biashara lakini wanakosa mtaji kutokana na kutotimiza vigezo vya mikopo ya taasisi za fedha. Kupitia mikopo hii ya Halmashauri tunaendelea kufungua milango ya fursa na kupunguza umaskini kwa wananchi wetu,” alisema Mhe. Koka.
Mbunge huyo amebainisha kuwa zaidi ya Shilingi bilioni 4.5 ziko katika mzunguko wa mikopo iliyotolewa na Halmashauri, hali inayochochea ukuaji wa biashara, kuongeza ajira na kupanua wigo wa mapato ya ndani ya Manispaa.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Mhe. Nickson Simon John, aliwataka wanufaika kuwa na nidhamu ya matumizi ya fedha na kuhakikisha mikopo hiyo inatumika kwa malengo yaliyokusudiwa.
“Fedha ni kama damu katika uchumi. Zinapozunguka kwa usahihi huleta uhai wa biashara, huongeza uzalishaji na kuinua maisha ya wananchi. Ni muhimu mikopo hii ikatumike kwa shughuli za maendeleo badala ya matumizi yasiyo na tija,” alisema.
Awali, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha, Dkt. Rogers Shemwelekwa, amesema kuwa katika mwaka wa fedha 2025/2026 Halmashauri tayari imetoa jumla ya Shilingi bilioni 2.1 kwa vikundi 457 vya makundi maalum.
Amefafanua kuwa kati ya fedha hizo, Shilingi bilioni 1.09 zimetolewa kwa vikundi 275 vya wanawake, Shilingi milioni 904.5 kwa vikundi 161 vya vijana na Shilingi milioni 158.8 kwa vikundi vya watu wenye ulemavu.
Utoaji wa mikopo hiyo unaendelea kuthibitisha dhamira ya Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha ya kutumia mapato ya ndani kuwawezesha wananchi kiuchumi, kuongeza ushiriki wao katika shughuli za uzalishaji na kujenga msingi wa maendeleo jumuishi yanayowanufaisha makundi mbalimbali ya jamii.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...