Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Zanzibar inakusudia kuimarisha uhusiano na ushirikiano na Jamhuri ya Singapore kwa kuelekeza nguvu zaidi katika diplomasia ya uchumi, biashara na uwekezaji.

Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo tarehe 10 Juni, 2026 Ikulu alipofanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Singapore, Mhe. Tharman Shanmugaratnam, Ikulu Zanzibar ambapo alizikaribisha kampuni na wawekezaji wa Singapore kuwekeza Zanzibar katika sekta za uchumi wa buluu, utalii, nishati, teknolojia na kuongeza thamani ya mazao ya baharini na mwani.

Kwa upande wake, Rais Tharman Shanmugaratnam amepongeza hatua kubwa za maendeleo zinazofanywa Zanzibar na kuahidi kuhamasisha wawekezaji wa Singapore kuja kuwekeza Zanzibar.

Baada ya mazungumzo hayo, Rais Dkt. Mwinyi, alimwandalia mgeni wake, Rais Tharman dhifa ya chakula cha mchana iliyofanyika Ikulu Zanzibar.








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...