Vijana katika mikoa tisa nchini wanatarajiwa kunufaika na Programu ya Mifumo Himilivu ya Chakula inayotekelezwa na Wizara ya Kilimo kwa lengo la kuongeza ushiriki wao katika sekta ya kilimo kupitia matumizi ya teknolojia za kisasa na miradi ya umwagiliaji inayotarajiwa kuanza mwaka ujao.

Akizungumza na waandishi wa habari Juni 22, 2026, wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma jijini Dodoma, Mtaalamu wa Masuala ya Vijana, Laurean Masele, amesema programu hiyo inalenga kuwajengea vijana uwezo wa kujiajiri na kuongeza kipato kupitia kilimo chenye tija.

Amesema mikoa inayonufaika na programu hiyo ni Tanga, Arusha, Kilimanjaro, Dodoma, Pwani, Morogoro, Njombe, Iringa na Mbeya, ambapo vijana wanahamasishwa kujiunga na shughuli za kilimo cha kisasa kupitia halmashauri za maeneo husika.

Masele amesema programu hiyo imeweka mkazo kwenye kilimo cha mazao ya bustani kama nyanya na vitunguu ambavyo hukomaa kwa muda mfupi na kuwawezesha vijana kupata kipato kwa haraka.

Aidha, utekelezaji wa skimu za umwagiliaji pamoja na uchimbaji wa visima kwa wakulima wadogo unatarajiwa kuongeza upatikanaji wa maji kwa shughuli za kilimo na kuifanya sekta hiyo kuwa ya kuvutia zaidi kwa vijana.

Ameeleza kuwa hatua hiyo ni sehemu ya juhudi za serikali za kubadilisha mtazamo wa vijana kuhusu kilimo na kukifanya kuwa chanzo muhimu cha ajira na maendeleo ya kiuchumi.



Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...