Cambridge, Uingereza Mkurugenzi Mtendaji na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna, amesema hatua inayofuata ya ukuaji wa Afrika itategemea taasisi zinazoaminika, mitaji ya muda mrefu na mifumo jumuishi, baada ya kuwasilisha hadithi ya mageuzi ya sekta ya benki Tanzania katika Cambridge Africa Business Conference 2026.

Akizungumza katika kongamano hilo lililoandaliwa na Cambridge Judge Business School, University of Cambridge, chini ya kaulimbiu ya “Kujenga Mustakabali wa Afrika: Mitaji, Ubunifu na Ukuaji wa Pamoja wa Bara la Afrika,” Zaipuna aliitumia safari ya NMB kama mfano wa taasisi ya Afrika inayoweza kuvutia mtaji, kuchochea ubunifu na kujenga uaminifu.

“Mustakabali wa Afrika hautaletwa kwetu na wengine; utajengwa na sisi wenyewe kupitia mifumo jumuishi, taasisi zinazoaminika na nidhamu ya kuleta matokeo chanya na endelevu kwa vizazi vijavyo,” alisema.

Zaipuna alieleza mageuzi ya NMB kutoka matawi 97, wateja takribani 600,000 na amana za Sh bilioni 150 mwaka 1997 hadi zaidi ya wateja milioni 10 leo. Alisema kati ya mwaka 2021 na 2025, NMB imewekeza zaidi ya Sh bilioni 230 katika miundombinu ya kidijitali, usalama wa mifumo, teknolojia za kiotomatiki na uwezo wa matumizi ya takwimu, huku zaidi ya asilimia 98 ya miamala yote sasa ikifanyika nje ya matawi kupitia njia za kidijitali na mbadala.

Katika mjadala huo, Mtaalamu wa Fedha (Structured Finance) kutoka AfDB, Eghosa Giwa Osaige, alisema kuimarisha uaminifu na kupunguza gharama za vihatarishi ni muhimu katika kuongeza mtiririko wa mitaji kuelekea Afrika.

Mkurugenzi wa Uwekezaji wa BII, Jumai Hadiza Mohammed, alisema hati fungani za kijamii na uendelevu za NMB zinatoa mfano imara kwa benki za Afrika kuhusu namna ubunifu, ubia na masoko ya mitaji vinavyoweza kufungua uwekezaji kwa kiwango kikubwa.


Mkurugenzi Mtendaji na Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB Bank Plc, Ruth Zaipuna, akitoa hotuba kuu katika Cambridge Africa Business Conference 2026 katika Chuo Kikuu cha Cambridge, ambako aliwasilisha safari ya mageuzi ya NMB na mchango wake katika uchumi wa Tanzania.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...