Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Serikali itaendelea kushirikiana na taasisi na wadau mbalimbali wa sekta ya afya ili kuimarisha utoaji wa huduma bora za matibabu kwa wananchi.
Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo, tarehe 11 Juni 2026, Ikulu Zanzibar, alipokutana na ujumbe wa Taasisi ya Humaniti ukiongozwa na Mtendaji Mkuu wake, Bw. Firaaz Azeez, pamoja na Mwanzilishi wa Doris Mollel Foundation, Bi. Doris Mollel.
Amesema Serikali inathamini mchango wa Taasisi ya Humaniti katika kuimarisha sekta ya afya kupitia uwekezaji katika rasilimali watu, miundombinu na vifaa tiba, huku akisisitiza umuhimu wa kuimarisha mifumo endelevu ya afya badala ya kutegemea programu za muda mfupi.
Aidha, Rais Dkt. Mwinyi ameishukuru Taasisi ya Doris Mollel Foundation kwa juhudi zake za kusaidia huduma za afya kwa watoto wachanga na watoto wanaozaliwa kabla ya wakati, hatua inayochangia kuokoa maisha ya watoto hao.
Katika hatua nyingine, Taasisi ya Humaniti imemkabidhi Rais Dkt. Mwinyi hundi ya shilingi milioni 503 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba vya uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo kwa watoto.
Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa Humaniti, Bw. Firaaz Azeez, amepongeza maendeleo makubwa ya sekta ya afya Zanzibar baada ya kutembelea Hospitali za Lumumba, Chumbuni na Magomeni.


.jpeg)

.jpeg)


.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)


.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...