RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametoa usafiri wa ndege kwa ajili ya kuwachukua mashujaa wa Timu ya Taifa ya Vijana chini ya umri wa Miaka 17 (Serengeti Boys), baada ya kufuzu kucheza fainali ya Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Vijana (AFCON U-17, 2026).
Ndege hiyo itaondoka leo, Juni Mosi, 2026, saa 5:00 usiku, kuelekea nchini Morocco, na itarejea Jumatano tarehe 03 Juni 2026.
Msafara huo utaongozwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda akiwa ameambatana na viongozi wa Serikali pamoja na Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu (Taifa Stars), lengo ikiwa ni kuongeza nguvu, morali na hamasa kwa Serengeti Boys katika hatua hiyo muhimu.
Waziri Makonda amemshukuru Rais Samia kwa kuendelea kuwekeza katika maendeleo ya michezo nchini pamoja na uamuzi huo wa kurahisisha safari ambayo itaongeza hamasa kwa vijana na kuimarisha uzalendo. Pia amewasisitiza Watanzania
kuendelea kuiunga mkono, kuishangilia na kuiombea heri Serengeti Boys katika fainali dhidi ya Senegal.
Mchezo huo wa fainali utachewa Juni 02 2026 nchini Morocco, saa 4:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki, ukiwa ni mchezo wa kihistoria kwa Tanzania na unatarajiwa kuvuta hisia za mashabiki wengi barani Afrika.
Aidha, Taifa Stars itatumia fursa hiyo kushiriki michezo ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya timu zitakazokuwa kwenye kalenda ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA), kama sehemu ya maandalizi ya mashindano yajayo.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...