Na Karama Kenyunko, Michuzi TV
SERIKALI imeahidi kuendelea kuimarisha na kutekeleza huduma za uzazi wa mpango pamoja na afya ya uzazi, mama, mtoto na vijana ili kuhakikisha mafanikio yaliyopatikana kupitia Mradi wa Scaling Up Family Planning (SuFP) yanaendelea kudumu hata baada ya mradi huo kufikia tamati.
Kauli hiyo imetolewa mkoani Dodoma na Mganga Mkuu wa Serikali, Dkt. Grace Magembe, kwa niaba ya Waziri wa Afya, wakati wa kongamano la kujifunza na kutathmini mafanikio ya Mradi wa SuFP lililofanyika jijini Dodoma baada ya utekelezaji wa miaka tisa.
Dkt. Magembe amesema serikali imejipanga kuhakikisha huduma hizo zinaendelea kutolewa kwa ubora katika ngazi zote za utoaji huduma kwa kuwa wananchi wanaendelea kuzihitaji bila kujali kama mradi umefungwa au la.
“Tunapozungumzia kufungwa kwa mradi, haimaanishi kufungwa kwa huduma. Watu wanaohitaji huduma bado wapo, hivyo jukumu letu kama serikali na wadau ni kuhakikisha huduma zinaendelea kutolewa kwa ufanisi na ubora uleule,” amesema.
Ameeleza kuwa serikali tayari imeonyesha dhamira yake kwa kuongeza mchango katika ununuzi wa bidhaa za uzazi wa mpango sambamba na kuzijumuisha katika mipango na bajeti za afya ili kuhakikisha upatikanaji wake unaendelea bila kukwama.
Katika hatua nyingine, Dkt. Magembe amewataka Waganga Wakuu wa Mikoa (RMOs), Waganga Wakuu wa Wilaya (DMOs) na Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhakikisha huduma za afya ya uzazi na uzazi wa mpango zinaendelea kupewa kipaumbele katika mipango na bajeti za maendeleo.
Ameonya kuwa kutoweka kipaumbele kwa huduma hizo kunaweza kusababisha kuongezeka kwa mimba za utotoni, vifo vya uzazi, kuacha shule kwa wanafunzi na changamoto nyingine za afya ya uzazi.
“Wananchi hawajui kama mradi umeisha au kuna changamoto za fedha. Wanachojua ni kwenda katika kituo cha afya na kupata huduma bora. Hilo ndilo jukumu letu sote kuhakikisha linatimia,” amesema.
Pia amepongeza juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan, ambaye ni Bingwa wa Umoja wa Afrika katika Afya ya Mama, Mtoto na Mchanga, akisema mafanikio yaliyopatikana nchini yanapaswa kutumika kama mfano kwa mataifa mengine barani Afrika.

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...