Na Karama Kenyunko, Michuzi TV

Mkurugenzi wa Uendeshaji wa MSI Tanzania, Dkt. Stephen Mutegeki, amesema utekelezaji wa Programu ya Scaling Up Family Planning (SuFP) umeonyesha kuwa maendeleo makubwa yanawezekana pale wadau mbalimbali wanaposhirikiana katika kufikia malengo ya pamoja.

Akizungumza katika kongamano la kujifunza na kutathmini mafanikio ya programu hiyo lililofanyika jijini Dodoma, Dkt. Mutegeki alisema MSI Tanzania itaendelea kushirikiana na serikali na wadau wengine kuhakikisha mafanikio yaliyopatikana yanaendelezwa na kwamba huduma bora na zenye usawa za afya ya uzazi zinaendelea kuwafikia wananchi wote.

Kwa upande wake, Naibu Mkurugenzi wa Maendeleo wa Ubalozi wa Uingereza nchini Tanzania, Will Guest, alisema Serikali ya Uingereza itaendelea kuunga mkono juhudi za kuboresha afya ya uzazi na haki za wanawake na wasichana.

Alisema kupitia SuFP, zaidi ya wanawake na wasichana milioni 5.2 walifikia huduma za uzazi wa mpango, hatua iliyosaidia kuzuia zaidi ya vifo vya wajawazito 6,500 na mimba zisizotarajiwa milioni 8.3.

Akizungumza kwa niaba ya washirika wa utekelezaji, Mwakilishi Mkazi wa UNFPA nchini, Mark Bryan Schreiner, alisema mafanikio ya programu hiyo yamethibitisha kuwa maendeleo makubwa yanawezekana pale serikali, watoa huduma, washirika wa maendeleo na jamii wanaposhirikiana.

Kwa mujibu wa washirika hao, mafanikio yaliyopatikana kupitia SuFP yametokana na ushirikiano wa karibu kati ya Serikali na wadau mbalimbali, wakiwemo MSI Tanzania, UNFPA, Serikali ya Uingereza kupitia FCDO, EngenderHealth na Pathfinder International.

Programu ya SuFP iliyotekelezwa kuanzia mwaka 2017 hadi 2026 kwa ufadhili wa Serikali ya Uingereza kupitia FCDO, ilitekelezwa kwa ushirikiano wa Serikali ya Tanzania na taasisi za EngenderHealth, UNFPA, MSI Tanzania na Pathfinder International.

Mkurugenzi uendeshaji wa MSI Dkt. Stephen Mutegeki





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...