Na Janeth Raphael MichuziTv -  Bungeni Dodoma 

Serikali imesema imebaini kuwepo kwa vitendo vya ujanja ujanja katika sekta ya ajira nchini, hali inayochangia kukiuka sheria na taratibu za ajira pamoja na kuathiri haki za wafanyakazi.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano ya Kazi), Dkt, Eveline Munisi, ameeleza hayo leo Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Nyasa, John John Nchimbi, aliyetaka kufahamu mpango wa serikali wa kuwasaidia Kamishna wa Kazi ili waweze kuwa na programu maalum za kutoa elimu katika maeneo mbalimbali, hususan migodini, ili kuelimisha kuhusu madhara ya ajira za watoto wadogo.

Mbunge huyo pia alihoji juu ya changamoto ya wageni wanaofanya kazi nchini bila kuwa na uelewa wa kutosha wa sheria za kazi, akisisitiza umuhimu wa kupatiwa elimu ya msingi kuhusu taratibu hizo.

Akijibu hoja hizo, Naibu Waziri Dkt. Munisi amesema serikali imebaini uwepo wa baadhi ya watu wanaofanya udanganyifu katika mchakato mzima wa ajira, ambapo “vishoka” huwachukua wananchi na kuwapangisha kazi kinyume na sheria na taratibu zilizowekwa.

Amesema serikali ipo katika hatua za kuimarisha utoaji wa elimu kwa waajiri, taasisi na wadau mbalimbali ili kuhakikisha wanazingatia sheria za kazi na kulinda haki za wafanyakazi, hususan makundi yaliyo katika mazingira hatarishi.

Aidha, amesisitiza kuwa serikali haitasita kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya wote watakaobainika kujihusisha na vitendo hivyo vinavyokiuka sheria za ajira nchini.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...