Na Mwandishi Wetu 

NAIBU Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Ngwaru Maghembe ameshiriki Mkutano wa Dharura wa Mawaziri wa Utatu wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC Organ Troika) uliofanyika kwa njia ya mtandao kujadili hali ya usalama katika kanda.

Akimwakilisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Maghembe aliipongeza SADC kwa juhudi za kuimarisha amani, usalama na kusuluhisha migogoro inayoibuka katika kanda.

Aidha, alisisitiza kuwa Tanzania itaendelea kuunga mkono juhudi za SADC katika kuimarisha amani kwenye ukanda huo.

Utatu wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC inaundwa na Nchi za Malawi Mwenyekiti, Eswatini Mwenyekiti ajaye na Tanzania Mwenyekiti anayemaliza muda wake na ina jukumu la kulinda kusimamia na kuhakikisha amani, usalama na utulivu unatamalaki katika ukanda wa SADC.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...