Serikali imeziagiza Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA) na Soko la Bidhaa Tanzania (TMX) kuhakikisha mazao ya kimkakati yanayozalishwa na wanaushirika yanakusanywa na kuuzwa kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani kwa vyama vya ushirika pekee, badala ya wanunuzi binafsi.
Maagizo hayo yametolewa na Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. David Silinde, wakati akifunga Jukwaa la Tano la Maendeleo ya Ushirika Mkoa wa Dodoma Juni 6, 2026.
Mhe. Silinde amesema mfumo wa ushirika umeendelea kuthibitika kuwanufaisha zaidi wakulima, hivyo ni muhimu kuhakikisha mazao ya kimkakati yanauzwa kupitia vyama vya ushirika ili kuongeza tija na manufaa kwa wazalishaji.
Aidha, amezitaka COPRA na TMX kutafuta njia mbadala za kuboresha bei za mazao kufuatia malalamiko ya wakulima kuhusu bei za kuanzia kwenye minada kuwa ndogo na kutokidhi matarajio yao, amesema taasisi hizo zinapaswa kuhakikisha wakulima wanapata bei nzuri na zenye kuridhisha ili kunufaika ipasavyo na uzalishaji wao.
Naibu Waziri huyo amesema Serikali itaendelea kuboresha mazingira ya kisera na kisheria kwa lengo la kuimarisha sekta ya ushirika nchini, huku ikihakikisha wakulima wanazalisha mazao yenye ubora wa ushindani katika soko la ndani na la kimataifa.
Katika kuongeza upatikanaji wa mitaji, amezitaka benki hususan Benki ya Ushirika kutoa mikopo yenye riba nafuu kwa vyama vya ushirika na wanaushirika binafsi ili kuongeza uzalishaji na tija katika sekta ya kilimo.
Sambamba na hilo, ameitaka Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) kuhakikisha vyama vyote vya ushirika vinakaguliwa kwa wakati, huku akiitaka Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) kuongeza kasi ya usimamizi na ufuatiliaji wa vyama vya ushirika nchini.
Mhe. Silinde amesema ushirika ni nyenzo muhimu katika kukuza uchumi wa taifa, kuongeza ajira za kudumu na za muda mfupi pamoja na kuboresha maisha ya wananchi.
Aidha, ametoa onyo kwa baadhi ya wanaushirika wenye tabia ya kujinufaisha binafsi kwa gharama ya wanachama wengine kuacha mara moja vitendo hivyo, akieleza kuwa vinaweza kusababisha migogoro, chuki, wizi na kupoteza malengo ya msingi ya ushirika.
Amesisitiza kuwa ushirika una mchango mkubwa katika kuunganisha nguvu za pamoja, kulinda wakulima dhidi ya unyonyaji, kuchochea ubunifu na kuimarisha mafunzo ya pamoja kwa wanachama, jambo linalochangia maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini.

.jpeg)
.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...