Na Janeth Raphael MichuziTv - Bungeni Dodoma
Spika wa Bunge, Mussa Azan Zungu, ametoa onyo dhidi ya tabia ya utoro miongoni mwa baadhi ya wabunge na viongozi wa Serikali, akisema hali hiyo imezidi na kuanza kudhoofisha nidhamu pamoja na ufanisi wa shughuli za Bunge.
Akizungumza leo Bungeni jijini Dodoma, Spika Zungu amesema baadhi ya wabunge wamekuwa wakifika asubuhi kusaini mahudhurio kisha kuondoka, na baadaye kurejea jioni kwa ajili ya kusaini tena bila kushiriki vikao vya Bunge.
Amesema pia kuna wabunge wanaosaini mahudhurio kwa niaba ya wenzao ambao hawapo kabisa Bungeni, jambo alilolitaja kuwa ni ukiukwaji wa taratibu za Bunge unaostahili kuchukuliwa hatua za kisheria na kinidhamu.
“Kuna wanaokuja asubuhi, wanasaini na kuondoka. Jioni wanarudi kusaini tena. Wapo pia wanaowasainia wenzao ambao hawapo. Tunawafahamu wanaosaini na wanaosainiwa, na hatua za kibunge zinapaswa kuchukuliwa,” alisema Spika Zungu.
Aidha, amesema kuna kundi lingine la wabunge ambao hawaonekani kabisa katika shughuli za Bunge licha ya kutokuwa na sababu za msingi za kutokuwepo, hali aliyoeleza kuwa ni kudharau mamlaka ya Spika pamoja na wananchi waliowachagua.
Spika Zungu amesisitiza kuwa kuanzia Jumatatu ijayo hatarajii kuona tabia hizo zikiendelea, akibainisha kuwa Ofisi ya Katibu wa Bunge ina uwezo wa kufuatilia na kubaini mahali alipo kila mbunge wakati wa shughuli za Bunge.
Pia aliiagiza Wizara inayosimamia mawasiliano kushirikiana katika kuimarisha mifumo ya ufuatiliaji wa mahudhurio ya wabunge ili kudhibiti utoro huo.
Katika hatua nyingine, Spika alimwelekeza Waziri Palamagamba Kabudi kulifanyia kazi suala hilo kwa kuwa liko chini ya usimamizi wa ofisi yake.
Vilevile, alikemea utaratibu wa baadhi ya mawaziri na manaibu wao kuwa safarini kwa wakati mmoja, akisema hali hiyo husababisha kukosekana kwa uwakilishi wa Serikali ndani ya Bunge.
“Haipendezi Waziri kuwa kwenye ziara huku Naibu Waziri naye akiwa kwenye ziara wakati huohuo. Wapeane zamu ili mmoja awepo Bungeni wakati mwingine akiwa kwenye majukumu ya nje,” alisisitiza.
Kauli ya Spika imekuja wakati Bunge likiendelea na shughuli zake jijini Dodoma, huku akitaka nidhamu ya mahudhurio irejee na kila kiongozi kutimiza wajibu wake kwa wananchi.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...