KUTOKA RUKWA.

HALMASHAURI ya Manispaa ya Sumbawanga na Halmashauri ya Mji Tunduma zimeendelea kuimarisha ushirikiano wa kiutendaji kupitia ziara ya mafunzo iliyolenga kubadilishana uzoefu wa utoaji huduma kwa wananchi, usimamizi wa miradi ya maendeleo na uhifadhi wa mazingira kwa manufaa ya wananchi na maendeleo ya Taifa kwa ujumla.

Timu ya Uongozi na Wataalamu kutoka Halmashauri ya Mji Tunduma imefanya ziara hiyo katika Manispaa ya Sumbawanga Mkoani Rukwa ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Momba Elias Mwandobo akiambatana na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Tunduma Salum Kiyambi, Mkurugenzi wa Halmashauri Mariam Chaurembo, Waheshimiwa Madiwani pamoja na wataalamu kutoka sekta mbalimbali.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo Mwandobo amesema kubadilishana uzoefu kati ya Halmashauri ni njia muhimu ya kuongeza ufanisi wa utendaji kazi na kuharakisha maendeleo ya wananchi kwa kujifunza mifano ya mafanikio inayotekelezwa katika maeneo mbalimbali Nchini.

Katika ziara hiyo wajumbe wametembelea miradi mbalimbali ya kimkakati inayotekelezwa katika Manispaa ya Sumbawanga ikiwemo Mradi wa Soko la Kimataifa la Mazao Kanondo, Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) Rukwa pamoja na Uwanja Mpya wa Ndege wa Sumbawanga ambao rasmi ulianza kutumika Juni 10, 2026 kwa safari za ndege kuelekea Tabora na Dar Es Salaam.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...