Jane Mwakyoma, Nkasi -Rukwa.
WILAYA ya Nkasi mkoani Rukwa imeanza kuweka mikakati mbalimbli ya kukabiliana na ugonjwa wa Ebola kwa kutoa elimu kwa wananchi namna ya dalili zake na njia za kujikinga na ugonjwa huo.
Kaimu mkuu wa wilaya ya Nkasi ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Sumbawanga Nyakia Chirukile amezitaka Taasisi zote zinazotoa huduma kwa jamii kuhakikisha zinatoa elimu kwa wananchi kuhusu dalili za ugonjwa wa Ebola na njia za kujikinga na kuwa tayari kuchukua hatua endapo kutatokea mshukiwa wa Ebola.
Akizungumza katika kikao cha dharura cha kamati ya Afya ya msingi wilaya (DPHC) Chirukile amesema wilaya imeanza kampeni ya uhamasishaji kwa kuwashirikisha wadau mbalimbli wa Afya, Elimu, Dini na maofisa maendeleo ya jamii kutoka ngazi za vijiji mpaka wilaya ili kuhakikisha elimu ya ugonjwa wa Ebola inazifikia jamii zote.
“Nimewaita hapa makundi yote katika jamii, tuzijue dalili na jinsi ya kujikinga na Ebola lakini pia kutoa elimu kwenye jamii na kuweka mikakati ya kuchukua kama Wilaya hasa tunapopata wagonjwa na kupokea wageni katika Wilaya yetu”amesema Chirukile.
Aidha Ofisa Afya wa wilaya ya Nkasi Method Mwankejela amesema Zahanati za Kipili, Kizumbi, Namanyere, Kabwe na Justice Korongwe zimetengwa kwa ajili ya kupokea na kuhudumia wagonjwa wanaoshukiwa na ugonjwa huo.
Mwankejela amesema mpaka sasa hakuna mgonjwa anayeshukiwa kuambukizwa na ugonjwa wa Ebola na kuwataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari kwa wageni wanaoingia na kutoka nchini.
Kwa upande wao Sheikh Mustapha Lupa na Mchungaji Fidelis Maheke ambao ni wajumbe wa kamati ya amani ya wilaya ya Nkasi wameipongeza serikali kwa kuanzisha mkakati wa kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa hatari wa ebola ambapo wamesisitiza elimu kutolewa ya kutosha hasa maeneo ya mwambao mwa ziwa kama kabwe,korongwe,kirando,kala,Namansi na maeneo mengine ili jamii iweze kujikinga vyema na ugonjwa wa Ebola.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...