Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) imeeleza kuwa ina mchango mkubwa katika kuwawezesha watoto, vijana na watu wazima waliokosa fursa ya elimu ndani ya mfumo rasmi kurejea na kuendelea na masomo yao.
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Taasisi hiyo, Profesa Philipo Sanga, wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma Juni 22, 2026, kwenye maadhimisho ya Wiki ya utumishi wa Umma.
Ameeleza majukumu makubwa ya TEWW ni kushughulikia elimu ya watu wazima na elimu nje ya mfumo rasmi, sekta ambayo imekuwa muhimu katika kuwasaidia wananchi wengi kupata elimu na ujuzi unaohitajika katika maisha na maendeleo ya taifa.
Amesema takwimu zinaonyesha kuwa kati ya kila watoto 10 kwa baadhi ya maeneo, watoto wanne hawapati fursa ya kuanza shule, huku kundi kubwa la wanafunzi likikatisha masomo katika ngazi mbalimbali za elimu.
“Katika kila wanafunzi 100, takribani 31 hudondoka na kushindwa kuendelea na masomo kwa ujumla, zaidi ya wanafunzi laki nne kutoka shule za msingi na sekondari hudondoka kila mwaka na kukosa fursa ya kuendelea na elimu."
Amebainisha kuwa bila uwepo wa Taasis ya Elimu ya Watu Wazima, idadi kubwa ya wananchi wengi wangeshindwa kupata nafasi ya kurejea katika mfumo wa elimu na kufikia malengo yao.
Kwa mujibu wa Profesa Sanga, Taasisi hiyo inatekeleza miradi mbalimbali ya elimu ya msingi na sekondari nje ya mfumo rasmi, inayolenga kuwapa wananchi fursa ya kupata elimu, maarifa na ujuzi unaowawezesha kujitegemea na kuchangia maendeleo ya taifa.
Aidha, amesema TEWW kupitia Chuo cha Elimu ya Juu cha Elimu ya Watu Wazima hutoa programu za elimu kuanzia ngazi ya cheti, stashahada, shahada hadi shahada za uzamivu kwa lengo la kuandaa wataalamu wabobevu watakaosaidia maendeleo ya nchi.
Ameongeza kuwa katika kila mkoa kuna viongozi wa elimu ya watu wazima wanaosimamia shughuli za taasisi hiyo na kuhakikisha huduma zinawafikia wananchi katika maeneo mbalimbali.
Aidha ameeleza changamoto mbalimbali zinazowakabili wanafunzi ndiyo chanzo kikuu cha kudondoka kwao kielimu, hivyo taasisi hiyo imejikita katika kuwasaidia kurejea masomoni na kutimiza ndoto zao za elimu.
Kwa upande wa elimu ya juu, Profesa Sanga amesema Taasis ya Elimu ya Watu Wazima imefanikiwa kudahili zaidi ya wanafunzi 6,000 na kwamba zaidi ya wanafunzi 2,000 huhitimu kila mwaka, jambo linaloonyesha mchango mkubwa wa taasisi hiyo katika kuboresha sekta ya elimu nchini.
Profesa Sanga amesema kupitia banda la TEWW katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea Jijini Dodoma hadi Juni 23, wananchi wanaweza kupata huduma mbalimbali ikiwemo taarifa za udahili na matumizi ya mfumo wa kutunza takwimu za elimu nje ya mfumo rasmi.

.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...