Na Janeth Raphael MichuziTv - Bungeni Dodoma
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum imeeleza kuendelea kuimarisha mifumo ya malezi, maadili na ustawi wa watoto na familia kama msingi muhimu wa kujenga Taifa lenye nguvu kazi yenye tija na maendeleo endelevu.
Hayo yamebainishwa na Waziri wa Wizara hiyo, Dkt. Dorothy Gwajima, wakati akiwasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2026/27 bungeni, ambapo ameeleza kwa kina mikakati inayoendelea kutekelezwa na Serikali katika kuhakikisha watoto wa Tanzania wanalelewa katika misingi bora ya maadili, ulinzi na ustawi wa kijamii.
Dkt. Gwajima amesema Wizara yake ina jukumu la kuratibu na kusimamia masuala yote yanayohusu malezi, maadili, matunzo na ustawi wa watoto pamoja na familia, ambazo ni nguzo muhimu katika maendeleo ya Taifa.
Amefafanua kuwa malezi chanya ya watoto yanayoambatana na maadili mema ni msingi wa kujenga Taifa imara lenye jamii yenye nidhamu, mshikamano na uwezo wa kuchangia maendeleo endelevu ya kiuchumi na kijamii.
Ameongeza kuwa Serikali imeendelea kuratibu utoaji wa elimu ya malezi chanya kwa wazazi, walezi na vijana balehe ikiwa ni sehemu ya juhudi za pamoja za kupunguza na hatimaye kutokomeza vitendo vya ukatili dhidi ya watoto nchini.
Katika hotuba yake hiyo, Waziri Gwajima amesisitiza kuwa watoto ni rasilimali muhimu na mtaji wa Taifa, hivyo wanapaswa kulindwa, kupendwa na kuendelezwa katika misingi ya maadili na tamaduni za Kitanzania.
Amesema mazingira bora ya malezi yanapaswa kuanzia ndani ya familia ambayo ndiyo chimbuko la tabia, nidhamu na maadili ya mtoto, lakini amebainisha kuwa kutokana na changamoto mbalimbali zikiwemo umaskini wa kipato, migogoro ya kifamilia, ukatili na vifo vya wazazi au walezi, baadhi ya watoto hujikuta wakiishi katika mazingira hatarishi yanayowafanya kuhitaji huduma za malezi mbadala na ulinzi wa kijamii.
Ameeleza kuwa Serikali inaendelea kutekeleza Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto ya mwaka 2021/22 hadi 2025/26, ambayo inalenga kuhakikisha kila mtoto mwenye umri wa chini ya miaka minane anapata huduma jumuishi za malezi na makuzi ili kuongeza kiwango cha ukuaji timilifu kutoka asilimia 47 ya sasa hadi asilimia 90 ifikapo mwaka 2050 kama ilivyoainishwa katika Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
Amesema katika mwaka wa fedha unaoendelea, Wizara imeratibu uandaaji wa mfumo wa kitaifa wa kupima matokeo ya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto unaojulikana kama Early Childhood Development Scorecard, ambao utasaidia kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa viashiria vya maendeleo ya mtoto nchini.
Aidha, Serikali imeanzisha mfumo wa kukusanya na kuchambua takwimu na taarifa za afua za malezi na makuzi ya awali ya mtoto kupitia mfumo wa ECD Dashboard, unaounganisha mifumo ya sekta mbalimbali za Serikali na taasisi zake.
Mfumo huo unalenga kubaini na kufuatilia utekelezaji wa nguzo tano muhimu za malezi na makuzi ya watoto wadogo ambazo ni afya bora, lishe toshelevu, uchangamshi na ujifunzaji wa awali, malezi yenye mwitikio pamoja na ulinzi na usalama wa watoto. Waziri Gwajima amesema nguzo hizo zina umuhimu sawa katika kuhakikisha mtoto anapata makuzi bora yatakayomwezesha kuwa raia mwenye mchango chanya katika jamii na Taifa kwa ujumla.
Katika hatua nyingine, Dkt. Gwajima amesema Wizara imetoa mafunzo kuhusu mifumo hiyo kwa maafisa 227 kutoka ngazi za mikoa na halmashauri zote nchini, ambapo kati yao maafisa 17 walitoka ngazi ya Wizara, 26 kutoka mikoa na 184 kutoka halmashauri, hatua inayoonesha dhamira ya Serikali ya kuimarisha usimamizi na utekelezaji wa afua za malezi na makuzi kwa karibu zaidi.
Amesema Serikali itaendelea kuhakikisha kila mtoto nchini analindwa, anapata malezi bora na analelewa katika mazingira salama yatakayomuwezesha kukuza vipaji na uwezo wake kikamilifu ili kuchangia maendeleo ya Taifa la kesho.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...