Na Belinda Joseph- Dodoma.
Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) umeendelea kuwa nguzo muhimu katika kusogeza huduma za mawasiliano karibu na wananchi, hususan waishio maeneo ya vijijini yasiyo na mvuto wa kibiashara kwa kampuni za mawasiliano.
Akizungumza wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, Mhandisi Wilfred Charles kutoka UCSAF Juni 21, 2026, amesema ushiriki wao katika maadhimisho hayo unalenga kuielimisha jamii kuhusu majukumu na miradi mbalimbali inayotekelezwa na mfuko huo katika kuboresha huduma za mawasiliano nchini.
Amesema UCSAF kwa kushirikiana na Serikali imekuwa ikitoa ruzuku kwa watoa huduma za mawasiliano ili kuhakikisha huduma hizo zinafika katika maeneo ya vijijini ambayo kwa kawaida hayavutii uwekezaji wa kibiashara.
Ameeleza kuwa Mbali na ujenzi wa miundombinu ya mawasiliano, UCSAF pia inatekeleza mradi wa utoaji wa huduma za WiFi katika maeneo ya wazi, pamoja na kupanua usikivu wa Redio ya Taifa na redio za kijamii katika maeneo mbalimbali nchini, hatua hiyo inalenga kuhakikisha wananchi wanapata taarifa sahihi na huduma za habari kwa urahisi zaidi.
Katika sekta ya elimu, UCSAF imefanikiwa kufikisha vifaa vya TEHAMA katika shule zaidi ya 1,000 za msingi, sekondari na vyuo nchini, ambazo zimeunganishwa na huduma ya intaneti huku wanafunzi wakipatiwa kompyuta ili kuwajengea uwezo wa kutumia teknolojia za kidigitali na kuongeza ushindani wao katika uchumi wa kidigiti.
Aidha, amesema mfuko huo unaendelea kutoa mafunzo ya TEHAMA kwa walimu ili kuwawezesha kufundisha kwa ufanisi zaidi masomo yanayohusiana na teknolojia pamoja na kutumia mifumo ya kidigitali katika utekelezaji wa majukumu yao.
Mhandisi Charles amesema juhudi hizo zinaendana na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, hususan lengo la nne ambalo linaweka mkazo katika matumizi ya TEHAMA na kuongeza upatikanaji wa huduma za serikali kwa wananchi wa maeneo ya vijijini.
Kwa upande wa mafanikio ya mawasiliano, amebainisha kuwa tangu kuanzishwa kwa UCSAF, zaidi ya minara 2,000 ya mawasiliano imejengwa katika maeneo ya vijijini, pia mradi wa ujenzi wa minara 758 uliokamilika na kuzinduliwa na Rais Samia Suluhu Hassan umewezesha zaidi ya wananchi milioni 8.5 kupata huduma za mawasiliano.
Sambamba na hilo, UCSAF imeboresha teknolojia ya mawasiliano kwa kupandisha hadhi ya minara 304 iliyokuwa ikitoa huduma za 2G pekee na kuiwezesha kutoa huduma za 3G na 4G, hatua iliyoongeza kasi na ubora wa mawasiliano kwa wananchi wengi zaidi.
Mhandisi Charles amewakaribisha wananchi kutembelea banda la UCSAF katika maadhimisho hayo ili kupata elimu kuhusu huduma zinazotolewa na mfuko huo, pamoja na kutoa taarifa za maeneo ambayo bado hayajafikiwa na huduma za mawasiliano.
"Malengo yetu ni kuhakikisha kila Mtanzania, awe wa mjini au kijijini, anapata huduma bora za mawasiliano kwa usawa".

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...