NA MWANDISHI WETU
VETERANI wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), wamesema wataendelea kuenzi mchango mkubwa wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa CCM, Mkoa wa Dar es Salaam, marehemu Mohammed Mtulia.
Ahadi hiyo ilitolewa na Veterani Sadick Chamumi, kwa niaba ya Katibu wa Maveterani hao, Mkoa wa Dar es Salaam, walipofika nyumbani kwa marehemu Mzee Mtulia, Mtaa wa Muheza, wilayani Temeke, kuwasilisha rambirambi zao.
"Mzee Mtulia ameacha wasifu mkubwa, hivyo inabidi tujifunze kutoka kwake. Kwa niaba ya Mavetarani wa UVCCM, tunaipa pole familia na tutaendelea kushirikiana nayo,”almesema Chamumi.
Mzee Mtulia alifariki dunia Mei 5, mwaka huu, nyumbani kwake Mtaa wa Mkuranga B, wilayani Temeke.
Naye, Katibu Msaidizi wa Veterani wa UVCCM, Mkoa wa Dar es Salaam, Justy Mboke, ameeleza Mzee Mtulia enzi za uhai wake alifanya mambo makubwa, hususan kuimarisha mabaraza ya wazee kuanzia ngazi za tawi, kata, wilaya hadi mkoa.
“Mabaraza hayo mpaka hivi sasa yanafanya kazi. Sifa hiyo tutaiheshimu na kuienzi sisi veterani,” amesema.
Kwa upande wake, Katibu wa Baraza la Wazee wa CCM, Mkoa wa Dar es Salaam, Mzee Mohammed Mbonde, amewashukuru veterani kwa kuwasilisha rambirambi.
“Mzee Mtulia alifundisha upendo, uelewano, kuheshimiana, kuthaminiana na kuvumiliana. Haya ndiyo yalikuwa malezi yake kwetu,” amesema na kuongeza kuwa tukio hilo ni la udugu zaidi na upendo.
Amewaomba wazee hao kuendelea kushirikiana na kushikamana kwa kuwa uzee ni udugu, busara na hekima.
Msemaji wa familia ya marehemu Mtulia,ambaye ni mtoto wa marehemu, Athuman Mtulia, alishukuru veterani kwa kumuenzi Mzee Mtulia, kwa kuwa kitendo hicho kimeleta faraja katika familia.
Veterani ni watu wote ambao wakuliwa TANU Youth Legue na Afro Shiraz Party Legue, waliotikia wito wa Baba wa Taifa hayati Mwalimu Julius Nyerere kutaka vijana wajiunge na Jeshi jipya la Tanganyika mwaka 1964 na waliotembea kwa miguu kuunga mkono Azimio la Arusha.
Pia wale wote walioshiriki vita ya Kagera dhidi ya Fashti Nduli Amin na ambao walikuwa vijana wa CCM waliovuka umri kwa mujibu wa kanuni toleo la Mwaka 1978 ukomo wa kuwa kijana wa miaka 35 ni veterani wa Chama.
Dhumuni ni kutayarisha veterani vijana wa kuwa watetezi na walinzi wa CCM na serikali yake kwa vitendo ambapo kariri ya vetenari hao ni Ujamaa na Kujitegemea.

.jpeg)
.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...