WANANCHI Watakiwa kujikita zaidi katika Kusoma na Kujifunza zaidi Elimu ya Usalama Barabarani ili kuepuka ajali zisizo za lazima hususani kwa Watoto Mashuleni.
Akizungumza na Wanahabari Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi kutoka Chama cha Mbio za Magari (AAT) Najma Rashid amesema kuwa Chama hicho kwa kushirikiana na shirikisho la mbio za Magari duniani (FIA) kumekuwa na ushirikiano mzuri na wakaribu zaidi ili kuhakikisha programu ya mafunzo kwa ajili ya madereva pamoja na
watoto wa shule za sekondari na Misingi na wananufaika na Elimu ya Usalama barabarani ikiwemo kuzifahamu Alama za Barabarani, na Kuhakikisha wanarekebisha Miundombinu Barabarani (vivuko).
Hata hivyo amesema Mafunzo hayo yalianza mapema mwaka jana 2025 katika shule zilizopo Wilaya ya Kinondoni na hatimae kwa sasa ni Wilaya ya Ubongo na kusogea Wilaya ya Temeke Kwa Mwakani.
Pia ameeleza kuwa mwitikio umekuwa mkubwa zaidi kutokana na kupungua kwa ajali kwa watoto mashuleni na kwa Karibu wamekuwa wakipewa ushirikiano mkubwa na Askari wa Usalama Barabarani ambao ndio Wakufunzi katika Shule hizo.
Kwa Upande wa Mkufunzi wa programu hiyo ya Usalama Barabarani Askari sajenti Letcia Ishengoma kutokea traffic Makao Makuu amesema wamekuwa wakiendelea kutoa Elimu kila kona ikiwemo mashuleni,vijiwe vya bodaboda,stendi za mabasi ambapo tunatoa elimu ili watu waweze kubaini makosa kabla ya kutoa hukumu au adhabu ikiwemo faini na mengineyo pamoja na namna sahihi ya kutumia Alama za Barabarani.
Aidha amesema kuwa Jeshi la polisi litaendelea kutoa elimu ni Jambo endelevu ili kudhibiti tatizo mapema kabla ajali haijatokea hivyo programu hii inawanufaisha Wanafunzi Mashuleni ili kuwajengea uwezo wa kujua Alama za Barabarani na Kunusuru Ajali na vifo.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...